Takriban watu 60 wafariki katika mafuriko Afrika Kusini

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo baada ya mvua kunyesha katika mji wa bandari wa Durban na maeneo ya jirani ya Afrika Kusini...

0

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo baada ya mvua kunyesha katika mji wa bandari wa Durban na maeneo ya jirani ya Afrika Kusini katika jimbo la KwaZulu-Natal imepanda hadi 59, mamlaka ilisema Jumanne.

Wataalamu wa hali ya hewa nchini walitabiri mvua zitakazoleta uharibif Jumanne usiku lakini walitarajia mvua hiyo kupungua “kwa kiasi kikubwa” siku ya Jumatano.

“Watu wengi walipoteza maisha huku Ethekwini (kijiji cha Durban) pekee ikiripoti vifo 45,” huku wilaya ya iLembe” ikiripoti zaidi ya vifo vya watu 14” serikali ya mkoa ilisema katika taarifa yake.

Ilisema mafuriko hayo “yalisababisha uharibifu kwa maisha na miundombinu” iliyoathiri jamii zote na tabaka kutoka maeneo ya vijijini, vitongoji hadi maeneo ya kifahari.

“Hii ni athari ya kutisha ya mabadiliko ya tabianchi na inabidi serikali kuchukua hatua mwafaka,” alisema Rais Cyril Ramaphosa ambaye atazuru Durban siku ya Jumatano.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika alitoa “rambirambi za dhati kwa familia ambazo zimepoteza wapendwa wao kufuatia mafuriko makubwa” alisema kupitia Twitter.

Mvua iliyonyesha kwasiku nyingi ilisababisha mafuriko katika maeneo kadhaa, ikabomoa nyumba na kuharibu miundombinu katika jiji la kusini-mashariki, huku maporomoko ya ardhi yakilazimisha huduma za treni kusitishwa.

Idara ya kudhibiti majanga katika jimbo la KwaZulu-Natal, ambalo Durban ndio jiji kubwa zaidi, iliwataka watu kukaa nyumbani na kuamuru wale wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kuhamia maeneo ya juu.

Zaidi ya nyumba 6,000 ziliharibiwa, alisema waziri mkuu wa mkoa Sihle Zikalala.

Shughuli za uokoaji zikisaidiwa na jeshi, ziliwaondoa watu waliokuwa wamekwama katika maeneo yaliyoathiriwa.

Wanafunzi 52 wa sekondari na walimu ambao walikuwa wamezuiliwa katika shule ya upili ya Durban, walifanikiwa kusafirishwa kwa ndege hadi maeneo salama, mamlaka ya elimu ilisema.

Zaidi ya shule 140 zimeathiriwa na mafuriko hayo.

Vituo vya umeme vilikuwa vimefurika na usambazaji wa maji kukatizwa — na kwamba hata makaburi hayakuepushwa na uharibifu huo.

Jiji lilikuwa limetoka kukabiliana na ghasia mbaya Julai mwaka jana ambapo maduka makubwa yaliporwa na ghala kuchomwa moto, katika machafuko mabaya zaidi nchini Afrika Kusini tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi.

Kumekuwa na taarifa za uporaji, huku picha za televisheni zikionyesha watu wakiiba kwenye makontena ya mizigo.

Serikali ya mkoa ililaani “ripoti za uporaji wa makontena” wakati wa mafuriko.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted