Uber yasitisha huduma zake Tanzania

Yasema itarudisha huduma endapo mazingira ya biashara nchini humo yatakuwa raifiki

0

Kampuni ya Uber nchini Tanzania imetangaza kusitisha huduma zake za UberX, UberXL na UberX Saver nchini humo kuanzia leo Aprili 14, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Uber Tanzania imeeleza  kuwa kanuni za sasa za usimamizi wa sekta hiyo si rafiki nchini Tanzania na zimekuwa changamoto kubwa katika uendeshaji wa biashara ya usafiri, hivyo wanasitisha hadi hapo muafaka utakapopatikana.

“Huu ni wakati mgumu kwetu sote, lakini haina maana kwamba ndio mwisho wa kila kitu,” imeeleza kampuni hiyo ikiongeza kuwa “tuko tayari kushirikiana na mamlaka husika na kuwa na mazungumzo yatakayoleta tija.” Imeeleza taarifa hiyo

Uber Tanzania imewashukuru wateja wake ambao walikuwa wakitumia huduma zake tangu ilipoanzishwa takribani miaka sita iliyopita

Aidha Uber Tanzania imesema pamoja na wakati mgumu walionao hivi sasa, wako tayari kwa mazungumzo na mamlaka husika ili kujenga mazingira wezeshi ya kibiashara

“Huu ni wakati mgumu kwetu sote, lakini hii haina maana kwamba ndio mwisho wa kila kitu. Tuko tayari kushirikiana na mamlaka husika na kuwa na mazungumzo yatakayoleta tija na kujenga mazingira wezeshi na tutarudi na kuendelea na kukupa usafiri wa kutegemewa na wa uhakika ambao umekuwa ukiitumia, baada ya kujiridhisha kwamba mazingira ya kibiashara ni rafiki”.

Taarifa ya Uber kusitisha huduma zake ni mwendelezo wa changamoto katika sekta ya usafiri ambapo kutokana kupanda kwa bei za mafuta wafanyabiashara wa usafiri wamekuwa wakiishinikiza serikali kupitia upya nauli za mabasi ya mijini na safari ndefu.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted