Amuua mwenzake kisa kugombania dagaa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kugombania unga, dagaa pamoja na simu  iliyopelekea wawili hao kupigana kwa kutumia...

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia mkazi wa kijiji cha Bwembwela wilayani Muheza kwa tuhuma za kumuua, Eliasa Omari (55) kwa kumkata mapanga akidai kumuibia unga na dagaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kugombania unga, dagaa pamoja na simu  iliyopelekea wawili hao kupigana kwa kutumia mapanga.

“Aliyeuwawa aliyekuwa anafanya kazi katika shamba la mkonge” amesema amanda Jongo.

Kamanda Jongo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumapili Aprili 17, 2022 na kwamba mtuhumiwa yupo katika Hospitali ya Teule ya Muheza akipatiwa matibabu.

Amesema kuwa kumaibuka wimbi la wizi wa kuvunja kwenye maduka hivyo Jeshi hilo limeanzisha oparesheni mbalimbali.

“Kumekuwa na wimbi la uvunjaji maduka na waliokamatwa wamewataja wenzao. Walioibiwa tv na vitu vingine wafike ofisi za Jeshi la Polisi kwa ajili ya utambuzi wa mali zao” ameeleza Kamanda Jongo.

Kamanda Jongo amebainisha kuwa katika kuelekea katika msimu wa sikukuu ya Eid Jeshi la Polisi linaendelea operesheni za usalama barabarani ili wasafiri wanatumia barabara katika hali ya usalama

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted