Ndugai asema 2025 hatogombea tena ubunge

Ndugai ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 20 na kushika nafasi mbalimbali kama mwenyekiti wa Bunge, Naibu Spika na baadaye Spika, ametangaza uamuzi huo...

0

Aliyekuwa  Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Kongwa, Job Ndugai ametangaza kutogombea tena nafasi ya ubunge wa jimbo hilo lililopo jijini Dodoma katika uchaguzi mkuu ujao 2025. 

Ndugai ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 20 na kushika nafasi mbalimbali kama mwenyekiti wa Bunge, Naibu Spika na baadaye Spika, ametangaza uamuzi huo leo jana Jumapili tarehe 8 Mei 2022.

Uamuzi huo umekuja ikiwa ni miezi Michache kupita tangu alipojiuzulu Uspika tarehe 6 Januari 2022, baada ya kauli yake kuhusu Serikali kuendelea kukopa nje ya nchi kuibua mjadala na kushinikizwa na viongozi wa chama chake- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu.

Mara baada ya kujiuzulu CCM iliendesha mchakato wa ndani na aliyekuwa naibu spika, Dk. Tulia Ackson akapitishwa kuwania nafasi hiyo kisha akachaguliwa na wabunge kuwa Spika.

“2025 sitagombea nafasi ya ubunge tena nastaafu siyo kama nastaafu kwa kushindwa lakini ni jamabo ambalo tayari nilishalipanga muda mrefu uliopita hivyo tutaendelea kushirikiana kama ambavyo tunashirikiana sasa,” amesema Ndugai.

Kuhusu gari hiyo iliyonunuliwa kwa kuchangisha michango kwa wanumi wa kanisa hilio pamoja na watu mablimbali amesema anapongeza wote ambao wamehusika kupatikana kwa gari hiyo.

“Tunapaswa kufanya vitu vyetu wenyewe bila kutegemea mtu aje kutusaidia kwani hata maandiko yanasema tutakula kwa jasho lakini siyo kwa dezo kama yapo maandiko hayo basi inabidi viongozi wa dini waanze kutufundisha lakini mimi sijawahi kuyaona,” amesema

Aidha, amesema Watanzania wanapaswa kuondokana na habari ya kutegemea mtu kuja kuwafanyia mambo yao.

Naye Askofu wa Kanisa Aglikan Tanazania Dayoyosisi ya Mpwapw, Jacob Chimeledya, amesema ni aibu kuendelea kutegemea wahisani katika kila jambo.

“Ni aibu sisi Watanzania tulivyo na rasilimali za kutosha kuendelea kusubilia wahisani kutoka nje kufanyia mambo yetu ni aibu pia kiongozi wa serikali kuitangaza Tanzania kuwa ni masikini licha ya uwepo wa rasilimali za kutosha’” amesema Askofu Chimeledya.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka aliwapongeza waliofanikisha kupatikana kwa gari hiyo ambayo itatumika na kasisa hilo kutatua chanagmoto za usafiri kila linapo hitajika.

Mtaka alisema jambo ambalo limefanywa na waumini hao kununua gari bila kusubiri msaada ni jambo lakuigwa na watu wote.

“Lazima sisi kama waumini tuache kitu ambacho tutaendelea kukumbukwa na kanisa na kuwapa wepesi viongozi wa dini katika mahubiri yetu siyo kutunga uongoo kwenye maziko yetu,” alisema

Aidha, aliwataka vingozi wa dini kutumia nyumba zao za ibada kuelimisha masula mbalimbali ya kijamii ikiwemo zoezi la sensa ya watu na kamazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti 2022.

“Tanawashukuru viongozi wa dini kwa kutupa ushirikiano katika mambo mbalimbali ikiwemo wakati wa chanjo ya UVIKO-19 na sasa tunapokwenda kwenye sensa tunaoamba ushirikiano wenu wa kutosha kufanikisha zoezi hili,” alisema Mtaka

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted