Polisi wa Tanzania, watumia mabomu kuwatawanya wanafunzi waliofunga barabara mkoani Geita

Polisi mkoani Geita wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Buseresere waliofunga Barabara Kuu ya Bukoba-Mwanza baada ya gari la kampuni...

0

Polisi mkoani Geita wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Buseresere waliofunga Barabara Kuu ya Bukoba-Mwanza baada ya gari la kampuni ya Fikoshi kumgonga mwanafunzi na kufariki dunia papo hapo.

Mwanafunzi huyo wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Buseresere iliyopo wilayani Chato, Susan Lupuga aligongwa kwenye eneo la kuvuka barabara (Zebra) wakati akivuka kutoka shuleni kwenda nyumbani.

Lile gari lilikuwa mwendokasi wanafunzi wa kidato cha pili walitakiwa kurudi kwa ajili ya kusoma tukiwa hapa uwanjani shuleni tuliona Fikoshi ikiwa na speed wakati ambao wanafunzi wanavuka zebra gari ikashka breki ikashindwa ikampitia Susan akafa hapohapo” Thomas Kulwa amesema

 Wananchi wamesema alama za wavuka kwa mguu zilizopo eneo hilo hazisaidii kutokana na magari kupita kwa mwendo mkali na kuiomba Serikali kuweka matuta kwenye eneo hilo.

Mkazi wa Buseresere, Mary James amesema hii ni ajali ya tatu kutokea katika eneo hilo na kila wanapoomba yawekwe matuta hayawekwi na ndio sababu wameona wafunge barabara ikiwa ni njia ya kupaza sauti ili wasikike.

Makamu mkuu wa shule ya Sekondari ya Buseresere, Msasi Mashindi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Martha Mkupasi amekiri kutokea kwa ajali hiyo na kusema wanafuatilia kilio cha wananchi cha kutaka matuta katika eneo hilo.

Juhudi za kumpata kamanda wa Polisi mkoa wa Geita kuzungumzia ajali hiyo hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kutopokelewa na ofini pia hakuwepo.

Chanzo Mwananchi

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted