Mbowe aionya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Tanzania

Mwanasiasa mwiba wa siasa za upinzani nchini Tanzania, ameyasema hayo leo wakati akihutubia Baraza Kuu la Chadema, lililowakutanisha wajumbe takribani 400 jijini Dar es salaam.

0
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe ameitaka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini humo kuacha mara moja kuvigombanisha vyama vya siasa nchini humo kwa kumwambia kuwa ugomvi wao wa kisiasa na wanasiasa wenzake wataumaliza wao wenyewe.

Mbowe ambaye ni mwanasiasa mwiba wa siasa za upinzani nchini Tanzania, ameyasema hayo leo wakati akihutubia Baraza Kuu la Chadema, lililowakutanisha wajumbe takribani 400 katika viunga vya jiji la Dar es salaam.

“Na msajili wa vyama vya siasa nakuambia ndugu yangu acheni tena muache mara moja, acheni mkakati wenu wa makusudi wa kugombanisha vyama vya siasa acheni wanasiasa tupatane wenyewewe”- amesema Freeman Mbowe.

Kauli hiyo Mbowe aliielekeza moja kwa moja kwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza, aliyemtaka kupeleka salam kwa Msajili Jaji Francis Mutungi kwamba vyama vya siasa visipangiwe nini cha kufanya.

Aidha Mbowe amesema CHADEMA iko tayari kutoa ushirikianao na serikali iwapo watahitajika kutoa ushirikiano huo.

Mkutano huo hii leo mbali na wanachama wa CHADEMA pia umehudhuriwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wanasiasa, wanaharakati na wadau wa masuala ya sheria.

Kwa upande wake Naibu Msajili Nyahoza amekipongeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuitisha mkutano wa Baraza Kuu.

Nyahoza ambaye amemwakilisha Msajili wa Vyama vya Siasa amesema pamoja na pongezi hizo amekishauri Chama hicho kuhudhuria mikutano ya vyama vingine kama vinavyofanya kwao.

“Huwa ninaenda kwenye vikao vya wenzenu, sio wao wawe wanakuja tu, mimi nasema hivi kwa kuwa huwa naenda kwenye mikutano ya vyama vyote 19,” alisema Nyahosa.

Baraza Kuu la Chadema hii leo pamoja na mambo mengine litatoa uamuzi wa rufaa za wabunge 19, waliofukuzwa uanachama wa chama hicho wakiongozwa na Halima Mdee

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted