Dk.Stergomena:Lengo la mafunzo ya JKT kwa vijana si kuwaajiri bali kuwapatia stadi za maisha

Dk. Stergomena ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo leo ambapo amebainisha kuwa dhumuni la mafunzo yanayotolewa kwa vijana ni kuwapatia stadi za kazi na stadi...

0

Waziri wa Ulinzi nchini Tanzania , Dk. Stergomena Tax,  amesema si rahisi kuwapatia ajira vijana wote wanaopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kwamba lengo la mafunzo hayo si kuwaajiri bali kuwapatia stadi za maisha

Dk. Stergomena ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo leo ambapo amebainisha kuwa dhumuni la mafunzo yanayotolewa kwa vijana ni kuwapatia stadi za kazi na stadi za maisha, ili baada ya kumaliza muda wa mafunzo na kutumikia JKT, waweze kurejea kwao wakiwa raia wema, wenye uwezo wa kujitegemea na kulilinda Taifa.

“Nitoe rai kwa vijana wote wanaopata fursa za kupata mafunzo hayo kuzitumia stadi za kazi walizozipata kujiajiri na kujitegemea si rahisi kuwaajiri vijana wote,” amesema Dk. Tax.

Amesema vijana 45,047 wamefanikiwa kupata  mafunzo ya ukakamavu, stadi za kazi, kuwajengea uzalendo na umoja wa kitaifa katika operesheni Samia Suluhu Hassan.

Amesema mafunzo hayo yametolewa katika kambi mbalimbali za JKT kwa mujibu wa sheria ya kujitolea.

“Jumla ya vijana 25,503 kwa mujibu wa sheria wamepatiwa mafunzo na kati yao 19,544 ni wa kiume na 5,959 ni wa kike,” amesema.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted