Kenya: Wizara ya Afya yaonya kuhusu matumizi mabaya ya dawa ya kutuliza maumivu

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Mei 20, bodi hiyo ilibainisha kuwa umma ulikuwa ukitumia kupita kiasi Dawa ya Diclofenac, Steroidal Anti-Inflammatory (NSAID) kwa ajili ya kudhibiti maumivu.

0

Wizara ya Afya kupitia Bodi ya Famasia na Sumu (PPB) imetoa onyo kuhusu matumizi mabaya ya dawa moja maarufu ya kutuliza maumivu nchini.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Mei 20, bodi hiyo ilibainisha kuwa umma ulikuwa ukitumia kupita kiasi Dawa ya Diclofenac, Steroidal Anti-Inflammatory (NSAID) kwa ajili ya kudhibiti maumivu.

Ilisisitiza kuwa Diclofenac ikitumiwa kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu, inahusishwa na ongezeko la hatari ya kuganda kwa damu kwenye mishipa, hasa kwa wagonjwa walio na matatizo ya moyo au hali ya mzunguko wa damu au walio na sababu fulani za hatari ya moyo na mishipa.Watu wanaotumia dozi ya juu 150 mg kwa siku na kwa muda mrefu wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo na kiharusi.

Dawa hiyo haipendekezwi tena kwa wagonjwa walio na historia ya mshtuko wa moyo au kiharusi, kuziba kwa mishipa ya damu kwenye moyo au ubongo au wamefanyiwa upasuaji au wale wenye matatizo ya mzunguko wa damu ambayo huzuia mtiririko wa damu kwenye mwili na viungo.

Madaktari wanapaswa kutathmini hatari kabla ya kupendekeza dawa hiyo kwa watu wanaovuta sigara au walio na matatizo mengine kama vile shinikizo la damu, walio na mafuta kwenye damu au ugonjwa wa kisukari.

Bodi ya Famasia na Sumu (PPB) pia ilishauri umma dhidi ya kutumia dawa bila ushari wa daktari.

Bodi ya Famasia na Sumu (PPB) imepewa mamlaka chini ya Sheria ya Famasia na Sumu (Sura ya 244) kusambaza taarifa za bidhaa za matibabu kwa wataalamu wa afya na kwa umma ili kuendeleza matumizi ya busara ya dawa hizo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted