TAKUKURU nchini Tanzania yamshikilia Muuguzi anaedaiwa kusafirisha kilo 174.77 za dawa za kulevya 

Akizungumza na waadishi wa habar leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Florence Khambi, amesema kufuatia upekuzi uliofanyika nyumbani kwa mtuhumiwa, paketi 162 zenye...

0

Mamlaka  ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Tanzania imemkamata, Salum Shabani Mpangula (54), mkazi wa Mtaa wa Relini – Tabata, ambaye ni muuguzi msaidizi Karikoo Dispensary kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya.

Akizungumza na waadishi wa habar leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Florence Khambi, amesema kufuatia upekuzi uliofanyika nyumbani kwa mtuhumiwa, paketi 162 zenye unga uliodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya zilikutwa ndani ya viroba sita vilivyokuwa vimehifadhiwa chumbani kwa mtuhumiwa.

“ Na paketi moja ya unga huo ilikuwa imewekwa kwenye mfuko mweusi wa nailoni na kufichwa chini ya kitanda,”ameeleza Khambi.

Amebainisha kuwa taarifa ya uchunguzi wa kitaalam kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali imethibitisha kuwa paketi zote 163 zilikuwa na dawa za kulevya aina ya heroin, ambazo jumla yake ni kilogramu 174.77.

“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kisheria kukamilika. Khambi amesema wamekamata jumla ya kilogramu 877.217 za dawa za kulevya na kuzuia uingizaji wa kilogramu 122,047.085 na lita 85 za kemikali bashirifu nchini.

“Dawa  hizo ni heroin kilogramu 174.112 zilizowahusisha watuhumiwa wawili na bangi kilogramu 703.105, zilizowahusisha watuhumiwa sita ambao wote wamefikishwa mahakamani,” amesema.

Pia Khambi amesema wameteketeza jumla ya hekari 21 za mashamba ya bangi mkoani Arusha na jumla ya kilogramu 250.7 za dawa za kulevya aina ya heroin na cocaine ambazo mashauri yake yalimalizika mahakamani.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted