Huduma la LUKU nchini Tanzania kukosekana kwa saa mbili

Tanesco imesema huduma hiyo itakosekana kuanzia saa 6 usiku hadi saa 8 usiku nchi nzima ili kupisha maboresho ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wanaolipia kabla...

0

Shirika la Umeme nchini Tanzania (Tanesco) limesema wateja wa huduma ya ununuzi wa umeme kupitia Luku watakosa huduma hiyo kwa saa mbili kwa usiku wa Jumatano kuamkia siku ya Alhamisi Juni 9 mwaka huu.

Tanesco imesema huduma hiyo itakosekana kuanzia saa 6 usiku hadi saa 8 usiku nchi nzima ili kupisha maboresho ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wanaolipia kabla ya matumizi (Luku), kupitia mifumo iliyopo katika kituo cha kujikinga na majanga (Disaster Recovery).

Meneja Mwandamizi wa Tehama kutoka katika shirika hilo, Cliff Maregeli amesema kutokana na changamoto hiyo ya kiufundi wateja wanashauri kununua umeme wa ziada ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

“Maboresho ni muhimu na yanalenga kuongeza ufanisi kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme ili kuhudumia wateja wengi ipasavyo pale inapotokea hitilafu ya aina yeyote katika kituo chetu Kikuu Cha mfumo,” amesema Maregeli

Kwa uapande wake Msemaji wa Shirika hilo, Martini Mwambene ameshauri wateja kuzingatia taarifa hiyo ili kuruhusu maboresho hayo ya mfumo kufanyika.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted