Nchi 5 zachaguliwa kuhudumu katika Baraza la Usalama la UN

Nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wameshiriki katika uchaguzi huo uliofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ndani ya Baraza Kuu la...

0

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 09 juni 2022 limefanya uchaguzi na kuchagua Msumbiji, Ecuador, Japan, Malta na Uswisi kuingia kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mihula ya miaka miwili kuanzia tarehe 1 Januari mwaka 2023. 

Nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wameshiriki katika uchaguzi huo uliofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ndani ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo nchi ya Msumbiji ilipigiwa kura 192, Ecuador – 190, Uswizi – 187, Malta- 185 na Japani – 184

Wanachama hao wapya watachukua nafasi zinazokaliwa kwa sasa na India, Ireland, Kenya, Mexico na Norway.

Rais wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , Abdulla Shahid, ametangaza matokeo ya kura hizo baada ya wajumbe wa Baraza Kuu kupiga kura na kueleza mataifa hayo matano yamekidhi vigezo ya kuchaguliwa baada ya kuata theluthi mbili ya kura zinazohitajika na idadi kubwa zaidi ya kura.

Wanachama watano wapya wataungana na wanachama wengine watano wasio wa kudumu ambao ni nchi ya Albania, Brazil, Gabon, Ghana, na Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na wanachama watano wa kudumu ambao ni  China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura,Waziri wa Masuala ya mambo ya nje na ushirikiano wa Msumbiji Verónica Nataniel Macamo Dlhovo, ameeleza kuwa taifa lake linataka “kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi, mazungumzo ya kudumu na utatuzi wa migogoro ya amani kama njia ya wanayopendelea ili kufikia amani ya muda mrefu na endelevu.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani, Odawara Kiyoshi, alisema “kwa ujumla, Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa zina mambo mazito kuhusu jinsi Baraza la Usalama la sasa linapaswa kuwa” na kwamba, ndani ya juhudi hizo , watajaribu kushughulikia hali hiyo na Korea Kaskazini.

Kwa upande wake Ian Borg, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malta, alielezea vipaumbele vya nchi yake kwa muda wakaokuwa ndani ya Baraza la Usalama kuwa ni pamoja na “kuendeleza ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama, haswa linapokuja suala la kuwashirikisha wanawake katika michakato ya amani na usalama, inayoongoza katika masuala ya watoto na silaha. migogoro, na kuhakikisha ulinzi wa watoto unaoangazi mabadiliko ya tabianchi kama tishio lililopo ikijumuisha katika muktadha wa kupanda kwa kina cha bahari, na kusisitiza umuhimu wa kusoma na kuandika, kama zana ya kujenga amani na kuzuia migogoro, ni baadhi ya mambo tutakayozingatia.“

Baraza la Usalama lina nchi 15. Watano kati yao wanajulikana kama wajumbe wa kudumu ambao ni  China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani. Nchi hizi pia zina haki ya kupiga kura ya turufu.

Baraza Kuu, ambalo linajumuisha nchi zote 193 Wanachama wa Umoja wa Mataifa, huchagua wanachama 10 wasio wa kudumu ambao watahudumu kwa kipindi cha miaka miwili.

Karatasi za kupiga kura zilizo orodhesha majina ya nchi zote zilizowasilishwa katika uchaguzi hutolewa angalau saa 48 kabla ya kupiga kura. 

Ni lazima nchi zipate wingi wakura zisizopungua thuluthi mbili, au kura 128, hata kama zitashiriki bila kupingwa.

Wagombea mwaka huu walikuwa wakiwania viti vitano chini ya makundi matatu ya kikanda: 

•    Mbili kwa nchi za Afrika na Asia-Pasifiki, 

•    Moja kwa Amerika ya Kusini na Karibiani, na

•    Mbili kwa Ulaya Magharibi na Mataifa mengine.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted