Polisi kuchunguza kifo cha mwanafunzi aliyejinyonga kwa kutumia Tai

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo ni la Juni 4, mwaka huu na kijana huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali na...

0

Jeshi la Polisi mkoani Geita linachunguza kifo cha mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Dotto Biteko iliyopo Kata ya Igulwa wilayani Bukombe, Petro Peter (18), aliyekutwa amefariki nyumbani kwao ikidaiwa amejinyonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo ni la Juni 4, mwaka huu na kijana huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali na tai ya shule.

“Huyu mtoto wiki mbili kabla ya tukio hilo la tarehe 4, alikuwa ametoroka nyumbani na kwenda kusikojulikana, wazazi wakatoa taarifa kwa mwalimu mkuu, ambao walianza kushirikiana na mtendaji kumtafuta.

“Taarifa ilipofika kwa mtendaji wa Kata ya Igulwa wakaanza kumtafuta huyu mtoto na wakaambiwa atakapoonekana tu huyu mtoto wamjulishe mtendaji ili waweze kumkamata na kumpeleka shuleni,” alisema Kamanda.

Alisema Juni 4, mwaka huu asubuhi kijana huyo alionekana nyumbani kwao na wazazi wakaenda kumjulisha mtendaji wa kata kwamba mtoto amesharudi. Walivyorudi walikuta ameshajinyonga.

“Hatujui sababu ya yeye kujinyonga lakini vilevile hatujui kwa nini alitoka nyumbani kwa zaidi ya wiki mbili zilizopita,” alisema na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea kubaini chanzo halisi

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted