Kesi ya akina Mdee na wenzake kuunguruma leo

Mdee na wenzake wamekwenda mahakamani kupinga uamuzi wa chama hicho kwa kuwavua uanachama na wamefungua maombi Mahakama Kuu, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, wakiomba kibali cha...

0

Waliokuwa wanachama 19 wa Chadema na wabunge wa viti maalumu, waliovuliwa uanachama wa chama hicho, Halima Mdee na wenzake 18, leo wanatarajiwa kuchuana vikali kwa hoja za kisheria na chama hicho mahakamani wakati maombi yao yatakaposikilizwa.

Mdee na wenzake wamekwenda mahakamani kupinga uamuzi wa chama hicho kwa kuwavua uanachama na wamefungua maombi Mahakama Kuu, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, wakiomba kibali cha kufungua shauri la mapitio ya kuhusu uamuzi huo.

Sambamba na maombi hayo, pia wamefungua maombi ya zuio la muda dhidi ya ubunge wao kusubiri usikilizwaji na uamuzi wa maombi yao ya kibali cha kufungua kesi.

Maombi hayo yote yamepangwa kusikilizwa leo na Jaji John Mgetta na mawakili wa pande zote watachuana kwa hoja za kisheria.

Katika usikilizwaji wa maombi hayo, jopo la mawakili wa kina Mdee linaloongozwa na wakili Aliko Mwamanenge litakuwa na kibarua cha kuishawishi mahakama kuridhia amri ya zuio la muda dhidi ubunge wa wateja wao na pia kuridhia kutoa kibali cha kufungua shauri rasmi la kupinga kuvuliwa uanachama wao.

Lakini jopo la mawakili wa Chadema linaloongozwa na Peter Kibatala, litakuwa na kibarua kuishawishi mahakama kuwa haistahili kutoa amri hiyo ya zuio la muda dhidi ya hatua zozote zitakazoathiri ubunge wao wala kibali cha kufungua shauri la kupinga kuvuliwa kwao uanachama.

Mdee na wenzake walichukua hatua hiyo baada ya uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema kutupilia mbali rufaa zao za kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho, kuwavua uanachama November 27,2020.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted