Walioshiriki zoezi la Ushirikiano Uganda warejea

Ni zoezi la kijeshi lililofanyika siku 14 kuanzia Mei 28, ambalo huandaliwa na nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, likihusisha washiriki  kutoka majeshi na vitengo mbalimbali vya...

0

Kikundi cha Tanzania kilichoenda kushiriki zoezi la 12 la  Ushirikiano Imara 2022 nchini Uganda, kimerejea na kukabidhi bendera ya Taifa.

Ni zoezi la kijeshi lililofanyika siku 14 kuanzia Mei 28, ambalo huandaliwa na nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, likihusisha washiriki  kutoka majeshi na vitengo mbalimbali vya nchi wanachama kwa nia ya kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Mwakilishi wa Mkuu wa Kikundi, Kanali Johnson Kajela, amesema kikundi hicho kimefuzu vizuri shughuli zote zilizolengwa, ambazo ni kujifunza jinsi ya kukabiliana na ugaidi, uharamia baharini, kushughulika na majanga aina zote pamoja na kulinda Amani na kwamba kilikabidhi bender jana.

Washiriki wa kikundi cha Tanzania kilichoshiriki zoezi hilo ni kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted