Bashungwa: Shule ziwashirikishe wazazi kupanga michango ya shule kabla ya kuanza kutoza

Bashungwa amewaagiza wakuu wa shule na walimu wakuu wa shule kuwashirikisha wazazi, bodi za shule, kamati za shule na walezi kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

0

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amewaagiza wakuu wa shule nchini kuwashirikisha wazazi na walezi katika kupanga michango kabla ya kuanza kutoza.

Bashungwa amesema hayo leo Alhamisi Juni 16, 2022 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulyankulu (CCM), Rehema Migila.

Mbunge huyo alisema pamoja na Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi kwa elimu msingi bado kuna michango mingi ambayo ni kero kwa wazazi.

Ametoa mfano wa moja ya shule kijijini (hakuitaja) ya bweni ambayo wanafunzi wanatakiwa hadi kutoa mchango wa kitanda na kuna baadhi hadi chakula.

“Inapotokea mzazi ameshindwa kuchangia mtoto anaadhibiwa. Serikali inakauli gani kwa shule zinazotoa adhabu kwa wanafunzi ambao wameshindwa kulipa michango yao badala ya wazazi,”amesema Rehema.

Amesema kuwa upo mwongozo ambapo kamati za shule zinatakiwa kuwashirikisha wazazi na walezi.

“Ningependa kutoa maelekezo kwa walimu wakuu na wakuu wa shule kushirikisha wazazi ama walezi kupitia mwongozo ambao tumeutoa wa namna ambayo tunawashirikisha kwenye ile michango ambayo tunahitaji kuwashirikisha,”amesema.

Bashungwa amewaagiza wakuu wa shule na walimu wakuu wa shule kuwashirikisha wazazi, bodi za shule, kamati za shule na walezi kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted