Khaby Lame ndio mfalme wa TikTok baada ya kuwa na wafuasi wengi zaidi kwenye TikTok

Khabane ‘Khaby’ Lame sasa ana wafuasi wengi zaidi kwenye TikTok, akiwa na wafuasi milioni 142.8 wakati wa chapisho hili.

0
Khabane ‘Khaby’ Lame

Khabane ‘Khaby’ Lame sasa ana wafuasi wengi zaidi kwenye TikTok, akiwa na wafuasi milioni 142.8 wakati wa chapisho hili.

Mcheshi mwenye umri wa miaka 22 alimpiku Charli D’Amelio wa Marekani, ambaye ameshikilia rekodi hiyo tangu Machi 2020. Viigizo vya Khaby vya kile kinachoitwa “lifehacks” vimekusanya mamilioni ya watu kutazama video zake na kumfanya apate umaarufu duniani kote.

Baada ya kupoteza kazi yake kama mfanyakazi wa kiwandani mwanzoni mwa janga la UVIKO-19, Khaby alilazimika kurejea nyumbani kwa mzazi wake huko Turin, Italia.

Wakati wa vizuizi vya kitaifa, Khaby aliunda akaunti yake ya TikTok kama njia ya kuondoa uchovu.

Video zake za kwanza zilimshirikisha akicheza, kutazama michezo ya video na kutumia programu kwenye TiKTok ingawa si watu wengi waliotazama video hizo.

Hayo yote yalibadilika mnamo Novemba 2020 wakati moja ya video zake ziliposambaa.

Khaby alikuwa akijibu video ya mtumiaji mwingine wa TikTok kuhusu changamoto za maisha, Khaby alipoonyesha suluhu rahisi zaidi kwa tatizo hilo.

Kwa ishara zake za mikono na macho yake yaliyoonyesha kustaajabika, Khaby alipata fomula ya ushindi.

Idadi ya wafuasi wa Khaby ilianza kuongezeka kwa kasi na kufikia Aprili 2021 alikuwa amempiku Gianluca Vacchi kama Mwitaliano anayefuatiliwa zaidi kwenye TikTok.

Kufikia Julai 2021, Khaby alikuwa mtumiaji wa pili mwenye wafuasi wengi kwenye TikTok na alishikilia rekodi ya wafuasi wengi kwenye TikTok (wa kiume) baada ya kumpiku Zach King.

Khaby aliendelea kuongeza umaarufu kwa kasi, akikusanya wafuasi kwa kiwango cha wastani cha milioni tatu kwa mwezi, ikilinganishwa na milioni moja ya Charli D’Amelio.

Baada ya kuunda akaunti yake katika mwezi uleule ambao D’Amelio alipata wafuasi wengi zaidi, Khaby sasa amepanda hadi kilele cha TikTok katika kipindi cha miaka miwili.

Charli D’Amelio bado anashikilia rekodi ya wafuasi wengi wa kike kwenye TikTok.

Pia ana mataji ya Rekodi za Dunia za Guinness kwa kuwa mtu wa kwanza kufikia wafuasi milioni 50 kwenye TikTok na mtu wa kwanza kufikia wafuasi milioni 100 kwenye TikTok.

Kulingana na Khaby, umaarufu wake mkubwa unatokana na vichekesho vyake vinavyovuka vikwazo vya lugha.

“Ninazungumza lugha ya kimataifa ambayo kila mtu anaelewa,” aliiambia Forbes.

Khaby ameendelea kujikusanyia umaarufu baada ya kusaini ushirikiano na Hugo Boss na kushirikiana na klabu yake ya soka ya Juventus FC mwaka jana.

Pia ametimiza baadhi ya ndoto zake za utotoni baada ya kukutana na Lionel Messi na kutengeneza video na Zlatan Ibrahimović na Usain Bolt.

Kuna yeyote ataweza kumbandua Khaby Lame kama mfalme wa TikTok?

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted