Tanzania  kupitia miongozo kupunguza michango shuleni

Katika majadala huo, baadhi ya wabunge waliiomba Serikali itatue changamoto ya utitiri wa michango ya wanafunzi shuleni, ili azma yake ya kufuta ada kuanzia shule ya msingi hadi...

0

Wakati Serikali ya Tanzania ikiwa imefuta ada kwa wanafunzi ambapo sasa kuanzia shule ya awali hadi kidato cha sita ni bure, sasa  inajipanga kupitia upya miongozo ya kujiunga shule za sekondari na kidato cha tano na sita, ili kupunguza masuala yanayoongeza michango ya wanafunzi shuleni isiyo na tija. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda amesyasema hayo leo, wakati akijibu hoja zilizoibuliwa na baadhi ya wabunge katika mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali, kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.

Katika majadala huo, baadhi ya wabunge waliiomba Serikali itatue changamoto ya utitiri wa michango ya wanafunzi shuleni, ili azma yake ya kufuta ada kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha tano na sita kwa ajili ya kuwapunguzia mzigo wananchi, iwe na tija.

“Hii sehemu ya gharama ya kusoma, tutapitia miongozo yote. Tutashirikiana na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Hazina, kuangalia miongozo ili kusiwe na mzigo mkubwa ambao unakinzana na azma ya Rais Samia Suluhu Hassan, ya kutoa elimu bila ada,” amesema Prof. Mkenda.

AidhaProf. Mkenda amesema “tutafanya haraka kupitia Join Instructions (fomu za kujiunga) zote na kuangalia mizigo ipi imewekwa ambayo wabunge wamesema tumeondoa Sh. 70,000 ya ada, lakini gharama nyingi ziko sehemu nyingine. Tutafanya kazi kuhakikisha tunapunguza michango yote ambayo haina maana na tija.”

Prof. Mkenda amesema, katika bajeti ya 2022/23, Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), imetenga fedha kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wanaotoka katika kaya masikini.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted