Tozo ya ving’amuzi nchini Tanzania yapunguzwa

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Juni 2022/2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo wakati akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusiana na Muswada wa Sheria ya...

0

Serikali ya Tanzania imepunguza tozo ya ving’amuzi nchini kufikia shilingi 500 hadi shilingi 2000 kwa kadri ya matumizi ya mteja baada ya majadiliano na Kamati ya Bunge ya Bajeti.

Kabla ya majadiliano hayo tozo iliyopendekezwa katika makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya serikali 2022/23 ilikuwa shilingi 1,000 hadi shilingi 3,000.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Juni 2022/2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo wakati akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusiana na Muswada wa Sheria ya Fedha 2022.

Amesema Serikali ilipendekeza Sheria ya Posta na Mawasiliano ya kuanzisha tozo hiyo ya shilingi 1,000 hadi shilingi 3,000 kwa ving’amuzi itakayokuwa ikitozwa kupitia malipo ya vifurushi.

“Hata, hivyo baada ya majadiliano ya kina ilionekana kwamba kiwango hicho ni kikubwa”amesema Sillo

Amesema kamati ilipendekeza kuanza kutoza kati ya shilingi 500 hadi shilingi 2,000 na kwamba Serikali ilikubali pendekezo la Kamati.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted