Afariki kwa kuteketea kwa moto baada ya magari kugongana na kisha kuwaka moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ,Urlich Matei amesema ajali hiyo imetokea jana June 27, 2022 saa 12 asubuhi.

0

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine kunusurika katika ajali baada ya roli  lililobeba  shehena za mizigo likielekea jijini Dar  es Salaam  kuferi breki na  kugonga magari  manne na kisha kuwaka moto katika  mtelemko wa barabara kuu ya Mbeya-Iringa eneo la Pipe line Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ,Urlich Matei amesema ajali hiyo imetokea jana June 27, 2022 saa 12 asubuhi.

Amesema ajali hiyo ilihusisha roli la mizigo  likiwa linaendeshwa na Erick Ndasigwa (39) mkazi wa  Dar es Salaam  lilifeli breki na kisha kugonga magari manne likiwepo gari ndogo ambayo  dereva wake alipoteza maisha akiwa ndani ya gari.

Matei ametaja watu walionusurika katika ajali ani madereva akiwemo  aliyesababisha ajali , Erick Ntasigwa, Yunus Amos, Philimon Bartazali  na Abdafik Mohammed (29) mkazi wa jijini Mbeya na dereva wa Shirika Water Reed Tanzania

Matei amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mtelemko mkali uliopo kwenye eneo ilipotokea ajali

Matei ameomba Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kuangalia uwezekano wa kupanua miundombinu ya barabara kwa njia nne kutokana na kutumika katika usafirishaji wa shehena za mizigo kwenda nchi mbalimbali.

Wamesema  mara baada ya kufika eneo la tukio walikuta gari ndogo ikiwa imenasa chini ya roli la mizigo huku kukiwa na mwili wa mtu mmoja aliyeteketea kwa moto.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted