Miili ya familia ya watu sita waliouawa wazikwa usiku

Miili hiyo imezikwa kwa pamoja jana Jumapili Julai 3, 2022 , majira ya usiku, huku vilio na simanzi zikitawala

0

Miili ya watu sita wa familia moja waliouawa kwa kukatwa na kitu chanye ncha kali na watu wasiojulikana imezikwa katika Kijiji cha Kiganza, wilayani Kigoma mkoani Kigoma.

Miili hiyo imezikwa kwa pamoja jana Jumapili Julai 3, 2022 , majira ya usiku, huku vilio na simanzi zikitawala

 Watu hao waliuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana wakiwa nyumbani kwao wamelala huku watoto wawili, mmoja mwenye umri wa miezi mitatu na mwingine miaka minne wakijeruhiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Menrad Sindano alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku akisema kuwa Jeshi hilo limeanza msako wa kuwatafuta watuhumiwa waliofanya unyama huo.

Sindano alisema kuwa watoto waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Maweni

Wananchi walioshiriki  katika mazishi hayo waliiomba Serikali kuongeza vituo vya polisi ili kuimarisha ulinzi na usalama, huku wakitaka polisi waongeze juhudi katika kufanya ukaguzi kwa wageni wanaoingia mkoani humo kwani hivi sasa familia imeingiwa na hofu baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Watu hao sita wa familia ya Mussa Cheche waliuawa kwa kukatwa katwa sehemu mbalimbali za miili yao kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumapili Julai 3 mwaka huu wakiwa wamelala.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted