Wasichana wang’ara ufaulu wa masomo ya Sayansi kidato cha sita

Kwa upande wa watahiniwa waliofanya vizuri zaidi kitaifa katika mtihani huo kwenye masomo ya sayansi, wasichana wamekuwa kinara ambapo wako saba wote kutoka Shule ya Sekondari ya St....

0

Shule za Sekondari za Serikali, pamoja na watahiniwa wasichana, wameng’ara katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita. 

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa leo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Athuman Amasi, katika shule 10 bora kitaifa, shule za Serikali ziko saba huku za binafsi zikiwa tatu.

Shule iliyoshika nafasi ya kwanza katika orodha hiyo ni Kemebos, ya mkoani Kagera ambayo inamilikiwa na mtu binafsi, wakati ya pili ikiwa ni Kisimiri iliyopo Arusha, inayomilikiwa na Serikali, huku ya tatu ikiwa ni Tabora Boys (Serikali), ya nne Tabora Girls (Serikali), ya tano Ahmes iliyoko Pwani (Binafsi) na ya sita ni Dareda iliyoko Manyara (Serikali).

Shule iliyoshika nafasi ya saba ni, Nyaishozi kutoka Kagera (binafsi),ya nane Mzumbe kutoka Morogoro (Serikali), ya tisa Mkindi kutoka Tanga (Serikali), na ya kumi ni Ziba kutoka mkoani Tabora (Serikali).

Kwa upande wa watahiniwa waliofanya vizuri zaidi kitaifa katika mtihani huo kwenye masomo ya sayansi, wasichana wamekuwa kinara ambapo wako saba wote kutoka Shule ya Sekondari ya St. Mary’s Mazinde Juu, iliyoko mkoani Tanga, huku wa kiume wakiwa watatu kutoka Shule ya Tabora Boys, ya mkoani Tabora.

Katika orodha hiyo, wa kwanza ni Catherine Mwakasege, Lucy Magashi (wa pili), Muhewa Kamando (wa tatu), Minael Mgonja (wa nne), Norah Kidjout (wa tano), Jennifer Chuwa (wa sita), Pauline Mabamba (wa saba), Rachel Joachim Moshy (wa nane ) Kulwa Mbizo Elias (wa tisa) na Oscar Eliakim Marabe (wa 10).

Kwa upande wa watahiniwa 10 waliofanya vizuri katika masomo ya lugha na sanaa kitaifa, wavulana wako sita na wasichana wako wanne, ambapo wa kwanza ni Hamza Ngosse kutoka Shule ya Songea Boys, mkoani Ruvuma, wa pili Charite Chonza, kutoka Zakia Meghji ya Geita, wa tatu Zilabhela Kombwey, kutoka Kisimiri iliyoko Arusha.

Wa nne ni Mebo Mgaya, kutoka Shule ya Ahmes ya mkoani Pwani, wa tano Gilead Gwaselya, kutoka Tukuyu ya Mbeya, wa sita Albert Boniphace kutoka Kisimiri, Arusha. Wa saba Abdallah Mtawanyika kutoka Kemebos ya mkoani Kagera.

Aliyeshika nafasi ya nane ni Winfrida Sugoya, kutoka Ahmes ya mkoani Pwani , wa tisa Hassan Buruhani kutoka Musoma mkoani Mara na wa mwisho Erick Godvin Mlay, kutoka Dareda ya mkoani Manyara.

Amasi amesema watahiniwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 wamefaulu ambapo wasichana waliofaulu ni 52, 229 sawa na asilimia 98. 55 na wavulana waliofaulu ni 52, 229 sawa na asilimia 98.55.

Ameongeza kuwa ubora wa ufaulu kwa watahiniwa waliofaulu kwa daraja la kwanza,la pili na la tatu umeongezeka kwa asilimia 1.32 ukilinganisha na mwaka 2021

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted