Kenya: Rais Kenyatta awataja wakuu 142 wa mashirika ya serikali katika uteuzi wake wa mwisho

Huku kukiwa zimesalia wiki tatu tu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaoashiria mwisho wa muhula wake, Rais Kenyatta amefanya uteuzi wa watu 142 katika bodi za mashirika mbalimbali ya...

0
Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya

Huku kukiwa zimesalia wiki tatu tu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaoashiria mwisho wa muhula wake, Rais Kenyatta amefanya uteuzi wa watu 142 katika bodi za mashirika mbalimbali ya serikali.

Uteuzi huo umo katika toleo la hivi punde zaidi la Gazeti la Kenya lililochapishwa Julai 8. Ingawa kwa mujibu wa sheria, muda wa uteuzi huo mwishoni wa uongozi wake unaibua sintofahamu.

Tofauti na orodha ya awali, walioteuliwa hawajumuishi wanasiasa ambao mara nyingi hurejea kwenye uteuzi wanaposhindwa kunyakua viti vya kisiasa.

Teuzi hizo ni pamoja na uteuzi wa mabaraza ya vyuo vikuu mbalimbali vya umma, ambavyo vimekuwa vikifanya kazi bila muundo mzuri wa vyombo muhimu vya maamuzi.

Uteuzi huo unamaanisha kuwa Rais mpya atakuwa na nyadhifa chache za kuwazawadi wanaoanguka katika kinyang’anyiro cha kisiasa.

Uteuzi mwingi unadumu kwa miaka mitatu, ikimaanisha kwamba Rais mpya atalazimika kufanya kazi na walioteuliwa na Bw Kenyatta.

Miongoni mwa walioteuliwa ni Prof Karuti Kanyinga, ambaye ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Ufadhili wa Vyuo Vikuu kwa miaka mitatu.

Uteuzi huo ulitangazwa kwenye gazeti la serikali na Waziri wa Elimu George Magoha ambaye pia alimteua aliyekuwa bosi wa Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya (Knec) Mercy Karogo kuwa mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Usimamizi wa Elimu ya Kenya.

Felix Odimmasi na Joyce Wanjiru Kanja waliteuliwa kuwa wanachama wa baraza hilo.

Bw Kenyatta pia amemteua Prof Julius O Nyabundi kuwa mwenyekiti wa Knec kwa miaka minne.

Anachukua nafasi yake Dk John Onsati.

Bodi Mpya ya Kenya Co-operative Creameries itakuwa chini ya uenyekiti wa Anthony Lan Njoroge Mutugi kwa miaka mitatu ijayo.

Wateule wengine ni Joanne M Yelbert (Bodi ya Utalii ya Kenya), Nelson Ndirangu (Mamlaka ya Ushindani), Mohammed Amin Sheikh (Mamlaka ya Kudhibiti Bima), Stephen Kuria (Bodi ya Haki za Madini), na Eric Mungai (Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira).

Waziri wa Hazina ya Kitaifa Ukur Yatani alimteua Abdirahin H Abdi kuwa mwenyekiti wa Mamlaka ya Mafao ya Kustaafu.

Bw Yatani alimteua tena Richard Kiplagat kuwa mwenyekiti wa Mamlaka ya Mali Isiyodaiwa na Dennis Aroka kuwa mwanachama wa bodi ya Shirika la Reli la Kenya.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CMC Holdings Bill Lay ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Udhamini wa Sekta ya Maji huku Mbatia Kimani, Kevin O Opiyo, Musa Ndeto na Dkt Mary Wambui wakiwa wanachama.

Baraza la Chuo Kikuu cha Nairobi litaongozwa kwa muda wa miaka mitatu ijayo na Prof Miriam Were, ambaye atachukua nafasi ya Prof Julia Ojiambo.

Msomi mwingine mkongwe, Prof Shem Wandiga, ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga kwa miaka mitatu.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted