Tanzania: Rais Samia Suluhu afanya mabadiliko katika jeshi la polisi

Ramadhani Kingai ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai nchini (DCI)

0
Ramadhani Kingai, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amemteua na kumpandisha cheo aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  na kamanda wa polisi mkoani Kigoma (RPC) Ramadhani Kingai kuwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai nchini (DCI)
Kingai anachukua nafasi ya Camillus Wambura ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP).

Wambura alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime ilisema kuwa Kingai amehamishwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma akitokea Mkoa wa Kinondoni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano Julai 20, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Simon Sirro aliteuliwa kuwa mkuu wa Jeshi la polisi mwaka 2017 chini ya uongozi wa Hayati John Pombe Magufuli akichukua nafasi ya Ernest Mangu.

Samia pia amemteua Kamishina wa polisi (cp) Hamad Khamis Hamad kuwa kamishna wa polisi Zanzibar akichukua nafasi ya Kamishna wa polisi Awadgi Juma Haji aliyeteuliwa kuwa mkurugenzi wa operesheni makao makuu.

Uteuzi huo umeanza rasmi Julai 19, 2022 na wote walioteuliwa wanatarajiwa kuapishwa leo Julai 20 saa tano asubuhi katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted