Waziri wa Afya nchini Tanzania atoa siku 67 MSD ifumuliwe

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake, Rosemary Slaa.

0

Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu ameipa tahadhari bodi mpya ya wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) kuwa biashara ya dawa ni miongoni mwa biashara hatari hivyo wanapaswa kuwa makini wakati wa utendaji wao huku akiipa siku 67 kuifumua bohari hiyo kiutendaji.

 Amesema awali MSD ilifanya kazi zake vizuri na kuaminiwa na nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), hivyo ameagiza kurudishwa kwa mifumo ya tehama iliyosaidia kudhibiti mianya ya ubadhirifu ndani ya taasisi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake, Rosemary Slaa.

“Mnakabidhiwa MSD lakini poleni maana hili ni dude, dawa ni biashara. Hapa kuna biashara na watu wanataka wapate faida kubwa na ni miongoni mwa biashara hatari ikiwemo biashara ya silaha haramu. Nisiwatishe endapo mtatekeleza wajibu wenu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu mtaepuka mengi.

“Kuna mambo muhimu ya kufanya ili kuishi maono ya Rais Samia kama alivyoagiza MSD ifumuliwe. Mpaka Septemba 30 zoezi hili liwe limekamilika ili tuanze kwa robo mwaka ya mwisho, jazeni kwa muundo uliopo ili kazi ianze mara moja,” amesema.

Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai kuhakikisha wanapangua safu ya uongozi pamoja na wafanyakazi wengine wa chini huku akiipa jukumu bodi kuhakikisha inasimamia jukumu hilo.

“Tumeondoa wale wakuu wa Idara lakini sasa badilisheni kama kuna mfanyakazi amekaa kitengo muda mrefu miaka mingi badilisheni”

“Hapa MSD mnaweza kusema ni mkurugenzi kumbe hata mtu wa chini anayepokea barua anafanya ubadhirifu. Sitaki tuingie tena kwenye masuala ya ubadhirifu,” amesema Waziri Ummy.

Amesema amepata wakati mgumu katika kufanya uteuzi wa wajumbe wa bodi kutokana changamoto zilizopo katika taasisi hiyo.

Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi amesema MSD imekaa kwa takribani miezi minane pasipokuwa na Bodi hiy

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted