Wanafunzi 8 wafariki kwenye ajali mkoani Mtwara, Rais Samia atuma salam za pole

Ajali hiyo imetokea leo Jumanne Julai 26, 2022, baada ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Msingi ya King David iliyopo Manispaa ya mtwara Mikindani  kutumbukia shimoni.

0

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kufuatia vifo vya watu 10 wakiwamo wanafunzi wanane vilivyosababishwa na ajali ya basi la shule.

Ajali hiyo imetokea leo Jumanne Julai 26, 2022, baada ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Msingi ya King David iliyopo Manispaa ya mtwara Mikindani  kutumbukia shimoni.

Katika Salamu zake za pole alizoziandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia amesema; “Nimesikitishwa na vifo vya wanafunzi 8 wa shule ya msingi ya King David na watu wazima 2 vilivyotokea leo asubuhi huko Mtwara Mikindani baada ya gari la shule kutumbulikia shimoni. Nawapa pole wafiwa, Mkuu wa Mkoa na jamaa. Mwenyezi Mungu awarehemu marehemu na kuwaponya majeruhi”.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mtwara Nicodemus Katembo amesema kuwa Kwenye ajali hiyo taarifa zinaeleza kuwa watu waliofariki ni 10 ambapo Wanafunzi 8, dereva 1 na Muangalizi 1 huku majeruhi wakiwa 19.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted