Baraza la Tiba Asili lapiga marufuku utumiaji wa dawa ya Mkongo

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof. Hamisi Masanja Malebo, ametoa kauli hiyo leo Julai 27, 2022 mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

0

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini Tanzania, limepiga marufuku matumizi kwa binadamu dawa aina ya Hensha maarufu kama Mkongo, inayomilikiwa na kituo cha Nyasosi Traditional Clinic cha jijini Dar es Salaam na kuifutia usajili  dawa hiyo.

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof. Hamisi Masanja Malebo, ametoa kauli hiyo leo Julai 27, 2022 mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Profesa Malebo amesema, baraza katika uchunguzi wake lilibaini dawa iitwayo Hensha maarufu Mkongo, yenye usajili namba TZ17TM0027, ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume iitwayo sildenafil, kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erecto.

Alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted