Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kufanya ngono na mwanawe

Akitoa hukumu hiyo, hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Nzega, Godfrey Rwekite alisema kutokana na ushahidi kukamilika, mahakama imeridhia kumuhukumu kwa Masanja Shija kutumikia kifungo hicho...

0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Masanja Shija (58) baada ya kumkuta na hatia ya kufanya mapenzi na mwanawe wa kike aliyekuwa chini ya miaka 18.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Nzega, Godfrey Rwekite alisema kutokana na ushahidi kukamilika, mahakama imeridhia kumuhukumu kwa Masanja Shija kutumikia kifungo hicho cha miaka 30 jela ili liwe fundisho kwake na kwa wengine.

 Kwa mujibu mawakili wa serikali wakiongozwa na Jenipher Mandago waliieleza mahakama hiyo kuwa Desemba 2 mwaka 2021 majira ya usiku, Masanja Shija alifumaniwa akifanya mapenzi na mtoto wake wa kike mwenye umri chini ya miaka 18

 Baada ya Masanja kutiwa hatiani, mawakili hao waliomba apewe adhabu kali ili fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia ya ajabu kama hiyo.

Shija kabla ya kusomewa adhabu aliomba kupunguziwa adhabu akidai ana familia kubwa inayomtegemea. 

Pamoja na maombi yake Hakimu Rwekite alimhukumu kutumikia kifungo hicho cha miaka 30.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted