Baba ambaka na kumlawiti mtoto wake wa miaka 12 mara nne kwa siku tofauti

Hassan ametiwa hatiani kwenye kesi hiyo namba 70/2021 na Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro katika hukumu iliyosomwa na Hakimu Charles Woiso.

0

Mkazi wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiri mkoni Manyara nchini Tanzania bwana Salimu Hassan (42), amehukumiwa miaka 30 kwenda jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kike (12).

Hassan ametiwa hatiani kwenye kesi hiyo namba 70/2021 na Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro katika hukumu iliyosomwa na Hakimu Charles Woiso.

Hakimu Woiso amesema anatoa hukumu hiyo ili iwe funzo kwa wanaume wenye tabia ya kuwanajisi na kuwalawiti watoto wao wa kuwazaa kwa kuwafanyia vitendo hivyo vya kikatili.

Amesema mahakama hiyo inamtia hatiani Hassan baada ya ushahidi wa mtoto, mama wa mtoto, Mary Hassan (50) na taarifa ya daktari wa kituo cha afya Mirerani, kuonyesha alifanya kosa hilo.

Amesema mama wa mtoto huyo, Mary Hassan ambaye hivi sasa ni marehemu, awali alitoa ushahidi kuwa Hassan alimfanyia vitendo hivyo mtoto huyo alipowaacha alfajiri kwenda shambani kununua mboga Septemba 16 mwaka 2021.

Amesema baada ya kumkuta Hassan amelala kitandani na mtoto wake, alipiga kelele na alisaidiana na watu kuita polisi waliomkamata na kisha kumfikisha mahakamani.

 Amesema pia mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 alitoa ushahidi mahakamani hapo kuwa baba yake mzazi alimhadaa, kumbaka na kumlawiti mara nne kwa siku tofauti tofauti.

Hakimu huyo alisema ushahidi wa taarifa ya daktari umeonyesha mtoto huyo aliingiliwa ukeni na kwenye njia ya haja kubwa na kitu kilaini ambacho siyo kigumu.

Hata hivyo, mara baada ya mahakama ya wilaya hiyo kumtia hatiani Hassan alimuomba hakimu alipe faini ili asifungwe jela kwani ana watoto anawalea na kuwasomesha. 

Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo, Amilton Mosses amemuomba hakimu Woiso atoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe funzo kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo ya kufanya ukatili kwa watoto wao.

Mosses amesema mtoto huyo ameathirika kisaikolojia kutokana na kitendo hicho kwani kitamuathiri kwenye maisha yake hivyo apewe adhabu kali kwani makosa kama hayo yanaathiri watoto.

Hakimu Woiso baada ya kusikiliza pande hizo mbili ametoa hukumu kwa Hassan ya kwenda jela miaka 30 na endapo kuna upande haukuridhika na hukumu hiyo ukate rufaa

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted