Kifo cha Mwangosi kinavyozunguka kwenye vichwa vya Polisi Tanzania

Daudi Mwangosi aliuawa Septemba 2,2012 katika kijiji cha Nyololo mkoani Iringa, mbele ya Kamanda wa Polisi kipindi hicho mkoani humo Michael Kamuhanda, wakati polisi wapofika kwenye Ofisi ya...

0

Kaimu Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga (ASP) Jeremiah Zitta, amebainisha hayo leo kwenye mdahalo na waandishi wa habari mkoani Shinyanga, wenye lengo la kuimarisha mahusiano wakati wa majukumu yao pamoja na ulinzi na usalama.

Amesema waandishi wa habari bado wanamtanzamo hasi na Jeshi la Polisi sababu ya kifo cha mwenzao Daudi Mwangosi huko Iringa, makosa ambayo yalikuwa yakiutendaji dhidi ya askari mmoja, na kusababisha kuendelea kulichukia jeshi lote kuwa hawapo kwa ajili ya kulinda usalama wa wanahabari wanapokuwa katika majukumu yao.

“Nawaomba waandishi wa habari muondoe mtazamo hasi juu ya jeshi la polisi kufuatia kifo cha Daudi Mwangosi, hayo ni makosa ambayo yalifanywa na askari mmoja, bali tufanye kazi kwa ushirikiano na tuta walinda,”amesema Zitta.

Naye Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga, Leonald Nyandahu, amesema Jeshi la Polisi litaendelea kuimarisha mahusiano mazuri na waandishi wa habari, sababu wanategemea kwa baadhi ya majukumu hasa ya utoaji taarifa kuzuia uhalifu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC) Greyson Kakuru, amesema huo ni mdahalo wa pili na Jeshi la Polisi, ambao umelenga kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri hasa katika masuala ya ulinzi na usalama kwa wanahabari wanapokuwa katika majukumu yao.

Daudi Mwangosi aliuawa Septemba 2,2012 katika kijiji cha Nyololo mkoani Iringa, mbele ya Kamanda wa Polisi kipindi hicho mkoani humo Michael Kamuhanda, wakati polisi wapofika kwenye Ofisi ya CHADEMA ili kuwatawanya wasifungue tawi la chama chao katika kijiji hicho.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted