Polisi wamshikilia mtuhumiwa aliyepanga njama za mauaji mkoani Katavi

Jeshi la Polisi mkoani Katavi linamshikilia Machia Mbasa (65) kwa tuhuma za kudaiwa kulanjama za kujaribu kumuua Mabula Ntemange (37) huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

0

Jeshi la Polisi mkoani Katavi linamshikilia Machia Mbasa (65) kwa tuhuma za kudaiwa kulanjama za kujaribu kumuua Mabula Ntemange (37) huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Katavi Ali Makame Hamad, amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Lwafe wilayani Tanganyika mkoani humo, ambapo amesema mtuhumiwa amekua akimtuhumu Mabula kutoka kimapenzi na mke wake mdogo pia kuchukua kodi katika vibanda vyake vya biashara vilivyopo katika kitongoji cha Lwafe wakati yeye akiwa gereza la mahabusu Mpanda kwa tuhuma za mauaji.

Jeshi la Polisi baada ya kupokea taarifa hizo lilichukua hatua za haraka na kufanikiwa kuzima jaribio hilo kwa kumkamata mtuhumiwa.

Makame amesema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kupanga njama ya kufanya hivyo huku akieleza aliwakodi wauaji wawili kutoka Kaliua mkoani Tabora na baada ya kufika Mpanda walipokelewa na mtuhumiwa nakisha kuwaficha maporini wakati wakisubili kutekeleza mauaji hayo.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mtuhumiwa Mbasa amekua akituma ujumbe wa vitisho vya mauaji kwa njia ya simu kwa watu wengine wawili ambao ni Charles Lugembe na Dogani Malima wote wakazi wa kijiji cha Mwamkulu mkoani Katavi.

Kamanda amesema mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa watu anaoshirikiana nao kufanya mauaji na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted