Vijana wang’ara katika uchaguzi Kenya

Uchaguzi wa mwaka wa 2022 wa Kenya ulivutia idadi kubwa ya wanasiasa vijana wengi wakibwagwa huku wengine wakiwalambisha sakafu vigogo wa kisiasa.

0
Linet Chepkorir mwakilishi wa wanawake metule kaunti ya Bomet baada ya kupokea cheti chake.

Katika ulimwengu wa siasa, fedha, umaarufu, masomo na uzoefu wa kisiasa uchangia pakubwa kwa mtu kuchaguliwa katika nafasi yeyote ya kisiasa.

Hata hivyo kati ya mataifa 54 afrika, Kenya inazidi kubadili mkondo huo. Uchaguzi wa mwaka wa 2022 wa Kenya ulivutia idadi kubwa ya wanasiasa vijana wengi wakibwagwa huku wengine wakiwalambisha sakafu vigogo wa kisiasa.

Aidha wengi ambao wameibuka na kung’ara katika uchaguzi huu wanatokea ukanda wa Bonde la Ufa.

Wafahamu wawakilishi wenye umri mdogo zaidi:

Linet Chepkorir Maarufu Toto-Mwakilishi wa kike kaunti ya Bomet

Akiwa na umri wa miaka 24, Linet Chepkorir ameandikisha historia ya kuwa kiongozi wa kwanza kutangaza kutangaza kushinda katika uchaguzi wa mwaka 2022 nchini Kenya.

Chepkorir ambaye aliwania wadhifa wa mwakilishi wa wanawake kaunti ya Bomet kupitia chama cha naibu wa rais William Ruto cha United Democratic Alliance (UDA), alikosa mpinzani na kupelekea tume ya IEBC kumtangaza kuwa mwakilishi wa wanawake mteule wa jimbo hilo.

Toto jinsi anavyojulikana sana alikpata umaarufu aliposhinda tiketi ya UDA wakati wa kura za michujo wa vyama siasa.

Mwakilishi huyo wa wanawake aliwashangaza wengi baada yake kumshinda mwakilishi wa wanawake wa jimbo la Bomet anayeondoka Joyce Korir katika mchujo huo na kukabidhiwa tiketi ya chama cha UDA katika kaunti iliyo ngome ya naibu wa rais na chama chake.

Wakati wa mchujo huo Chepkorir alijipatia kura 242,775

Linet Chepkorir na naibu wa rais William Ruto aliposhinda mchujo wa chama cha UDA.

Wengine waliopoteza katika uchaguzi huo wa mchujo ni pamoja na Beatrice Chepkorir, Eddah Chepkoech, Faith Chepkirui, Cicilia Chepkoech, Brendah Chepng’etich, Eunice Cherono, Susan Koech, Stacy Chepkemoi na Joan Chepkirua.

“Asante sana kaunti ya Bomet kwa uungwaji mkono usio na kifani katika safari yangu ya kisiasa. Nitawafanyia kazi kama nilivyohaidi wakati wa kampeni,” alisema Toto.

Mwakilishi huo amefuzu na shahada ya usimamizi wa Biashara (Business Adminstration) kutoka chuo kikuu cha Chuka kaunti ya Meru na atahudumia kaunti ya Bomet kwa muhula miaka mitano ijayo.

Hata hivyo Toto alisema haijawa raihi kufika hapo alipofika ikizingatiwa kuwa alikuwa anachuana na wanasiasa wenye uzoefu na hela ambazo walitumia kufika kila sehemu ya kaunti na pia kununua umaarufu. “Nimekuwa na chamamoto chungu nzima katika kupiga kampeni yangu ambayo ilikuwa ya nyumba hadi nyumba has kwa kuwa sikuwa na fedha kinyume na wapinzani wangu ambao kwao fedhaa walikuwa nayo tena ya kutosha;” alisema Chepkorir baada ya kutangazwa kuwa mshindi.

Abraham Osoi Orikai

Mwakilishi wa kaunti mteule wadi ya Matapato kaskazini kaunti ya Kajiado Abraham Osoi Orikai.

Kando na Toto mwingine ni Abrahama Osoi Orikai pia anaingia katika orodha ndogo ya wanasiasa wachanga nchini leo hii.

Orikai mwenye umri wa miaka 24 alichaguliwa kama mwakilishi wadi wa Matapato kaskazini iliyoko kaunti ya Kajiado kupitia tiketi ya Wiper.

Osoi ambaye alisomea katika chuo kikuu cha KCA na ni mhasibu kitaaluma amerejelea zile changamoto ambazo alipitia katika safari yake hii ya kisiasa.

Alifanya kampeni za nyumba hadi nyumba pekee kutokana na uchache wa fedha za kufadhili shughuli zake ila alisalia makini na thabiti kuhusu safari yake ya kuwa mwakilishi wa wadi.

Mwakilishi huyo wa wadi mteule ambaye alichagua kugombea wadhifa huo kupitia chama cha Wiper katika eneo ambalo linadhamiwa kuwa na ufuasi mkubwa wa chama cha ODM, anasema amejitolea kupiga jeki suala la vijana uongozini kwa kuongoza muhula wake wa miaka mitano kwa njia bora.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi na afisa mkuu wa IEBC Mugo Ngunjiri, Osoi ametoa changamoto kwa vijana kujiunga na siasa na kutosubiri kupewa uongozi.

“Ninatoa shukrani zangu kwa mwenyezi Mungu na kwa wapiga kura wa wadi yangu. Nimefurahishwa  sana na uungwaji mkono ktoka kwa wapiga kura wa wadi yangu. Nataraji kuendelea kujibidiisha kuhakikishia wakenya kuwa viongozi wachanga wanaweza ongoza vyema,” alisema Osoi.

Amesisitiza kuwa kizazi kipya kina uwezo wa kutosha wa kubadili jinsi mambo yamekuwa yakifanywa na hata kushinda uchaguzi.

“Wapiga kura wakenya wanaamua kuheshimu demokrasia. Umati hauna maana tena kwa kuwa wapiga kura sasa wako makini katika kupiga kura na wanafanya uamuzi wa kujitegemea,”

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted