Rais Samia aendelea kupigia chapuo lugha ya Kiswahili

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, mkuu huyo wa nchi yupo Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kushiriki mkutano wa 42 wa nchi...

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametaka kuharakishwa mchakato wa kukipitisha rasmi lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha nne za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, mkuu huyo wa nchi yupo Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kushiriki mkutano wa 42 wa nchi za Jumuiya hiyo.

Akitoa maoni yake katika mkutano huo, Samia amesisitiza umuhimu kwa nchi wanachama kuzingatia uwiano wa jinsia katika ngazi za maamuzi, akibainisha kuwa Tanzania imejitahidi katika hilo.

“Nafasi hizo za uongozi serikalini na bungeni nchini Tanzania ni pamoja na Waziri wa Ulinzi (Dk Stergomena Tax), Mambo ya Nje (Liberatha Mulamula), Uwekezaji (Dk Ashatu Kijaji), Utalii (Dk Pindi Chana) na nafasi ya Spika wa Bunge (Dk Tulia Ackson),” amesema.

Katika hatua nyingine, amesisitiza umuhimu wa usalama wa chakula kwa nchi wanachama, huku akiyataka mataifa hayo kuwekeza kwenye uchumi wa buluu.

Hata hivyo, leo Rais Samia anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo, ambapo pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Felix Tshisekedi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted