Karani wa Sensa akutwa amelewa pombe huku akihesabu kaya moja siku nzima

Mratibu wa Sensa wa Manispaa ya Musoma, Joseph Ochora amemtaja karani wa sensa, Thomas Ndyetabura kwamba anashikiliwa na polisi tangu juzi  kwa kuhesabu kaya moja tu kutwa nzima,...

0

Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za  kujaribu kukwamisha zoezi Sensa ya Watu na Makazi mjini Musoma ambalo hivi sasa linaendelea nchi nzima..

Mratibu wa Sensa wa Manispaa ya Musoma, Joseph Ochora amemtaja karani wa sensa, Thomas Ndyetabura kwamba anashikiliwa na polisi tangu juzi  kwa kuhesabu kaya moja tu kutwa nzima, baadaye kukutwa akiwa amelewa.

Kwa mujibu wa Ochora karani huyo alitakiwa kuhesabu kaya kati ya 20 hadi 30 kwenye Kata ya Kwangwa, lakini baada ya matendo hayo nafasi yake ikatolewa kwa karani mwingine na kazi inaendelea.

Amesema kaya hiyo ina binti aliyemtaja kwa jina moja la Leila na mama yake mzazi (hakumtaja majina), kwamba licha ya kugoma kuhesabiwa, waliwatolea maneno ya kashfa karani wa sensa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Longinus  Tibishubwamu amethibitisha uwepo wa matukio hayo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted