Asilimia 99 ya Watanzania wamehesabiwa sensa ya watu na makazi

Mtakwimu Mkuu wa Serikali nchini Tanzania, Dkt Albina Chuwa hii leo amewaambia wanahabari kwamba hatua hiyo iliyobaki itakwenda kukamilika hadi tarehe 5 2022 September na zoezi hilo litafanyika...

0

Wakati zoezi la sensa likiendelea nchini Tanzania baada ya siku za kuhesabiwa kuongezwa, imeelezwa kuwa hadi kufikia leo Agosti 31,2022 asilimia 99.93 wamehesabiwa katika sensa ya watu na makazi iliyoanza Agosti 23 mwaka huu.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali nchini Tanzania, Dkt Albina Chuwa hii leo amewaambia wanahabari kwamba hatua hiyo iliyobaki itakwenda kukamilika hadi tarehe 5 2022 September na zoezi hilo litafanyika kwa njia ya simu zilizotolewa zitatumika kuwafikia ambao hawajahesabiwa .

”Sensa ya watu na makazi imebaki asilimia 0.07 kukamilisha zoezi ambapo zoezi hilo litaendelea hadi Septemba tano mwaka huu kwa kutumia namba za simu maalumu ambazo zilitolewa na zitatumika kuwafikia ambao hawajahesabiwa kwa utaratibu maalumu kupitia viongozi wa mitaa na vitongoji.”amesema Dk.Chuwa

Dkt Chuwa amesema kuwa  utaratibu Maalum utaandaliwa wa namna ya kuzifikia Kaya hizo kupitia Viongozi wa mitaa na vitongoji

“Kwa upande wa sensa ya majengo hadi kufikia leo asubuhi jumla ya majengo yaliyokwisha kuhesabiwa ni 6,351,927 ambapo taarifa za umiliki, mahali yalipo na taarifa nyingine zilizoizinishwa katika dodoso la majengo zimekusanywa.

Kwa makadirio ya operesheni anwani za makazi inategemewa kuhesabu majengo yapatayo milioni 12.7 nchi nzima.

Hata hivyo Dkt Chuwa amesema kuwa sensa ya majengo Dodoso lake linamaswali 27, taarifa zinazokusanywa zinazohusu aina na sifa za Majengo,idadi ya majengo na Nyumba (unit)zilizopo ,hali ya ujenzi /ukaazi na sababu za jengo kutumika.

” Kama tunavyofahamu Serikali kwa Mara ya kwanza tangu tupate Uhuru mwaka 1961 sensa ya Watu na makazi ya kidigitali ambayo imejumuisha sensa ya majengo na sensa ya Anwani za makazi katika Mfumo wake wa utekekezaji.”amesema 

Dkt Chuwa ameeleza kuwa sensa ya Watu na makazi hapa nchini hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya takwimu Sura 351 kifungua kidogo Cha 6(2)(a) sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 na kama ilivyokuwa sensa nyingine zilizokwisha kufanyika hutumia miongozo ya Umoja wa mataifa kwa Kuwa matokeo yake yanatumika kitaifa na Kimataifa.

“Kuhusu Bajeti ya sensa ya Watu na makazi na sensa ya Majengo inayoendelea nchi mzima kwamba Bajeti iliidhinishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 ni kiasi cha shilingi bilioni 400 sawa na wastani wa TSHs.6,265 au dola za kimarekani (USD) 2.7 kwa mtu mmoja,” amefafanua Dkt Chuwa

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted