Masauni: Suala la tendo la ndoa ni haki lakini si haki ya msingi tunayotoa kwa wafungwa

Masauni ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Viti maalum(CCM) Bahati Keneth Ndingo, aliyetaka kujua ni lini serikali itaanza kuruhusu wafungwa kupata haki...

0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nchini Tanzania, Mhandisi Hamad Masauni.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nchini Tanzania, Mhandisi Hamad Masauni amesema Haki ya faragha kwa wafungwa na wenza wao itaanza kutolewa nchini humo hadi pale ambapo mifumo ya ksheria na miundombinu ya magereza itakapokidhi kutolewa kwa haki hiyo.

Masauni ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Viti maalum(CCM) Bahati Keneth Ndingo, aliyetaka kujua ni lini serikali itaanza kuruhusu wafungwa kupata haki ya faragha na wenza wao

“Suala la tendo la ndoa ni haki lakini si haki ya msingi, haki ya msingi ambayo tunatoa kwa wafungwa ni chakula, mavazi, maradhi kwa hiyo kuna mambo mengi ya kuyazingatia ambayo yanapaswa kufanyika kwanza kabla ya kuruhusu haki hiyo ambayo mbunge anaipigania”

“Wakati mwingine inakua sio jambo jema kwa mila zetu na desturi kwamba kila mtu ajue kwamba sasa hawa wanakwenda kufanya tendo la ndoa”amesema Waziri Masauni

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted