Watu 38 wathibitika kuugua ugonjwa Surua nchini Tanzania

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Alhamisi Septemba 15,2022  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amezitaja halmashauri hizo kuwa ni Bukoba yenye sampuli tatu, Wilaya ya Handeni...

0

Wizara ya Afya nchini Tanzania imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa surua katika halmashauri saba nchini huku watu 38 wakithibitika kuwa na ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Alhamisi Septemba 15,2022  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amezitaja halmashauri hizo kuwa ni Bukoba yenye sampuli tatu, Wilaya ya Handeni sampuli nne, Kilindi tatu, Mkuranga nne, Kigamboni nane, Manispaa ya Temeke 12 na Manispaa ya Ilala nne.

“Mlipuko wa ugonjwa wa surua huthibitika baada ya sampuli tano za wahisiwa huchukuliwa kutoka wilaya moja ndani ya mwezi mmoja endapo sampuli tatu au zaidi kati ya hizo tano zilizochukuliwa zimetoa majibu chanya,” amesema Waziri Ummy.

Aidha, amesema katika kudhibiti ugonjwa huo, wizara inaendelea kuimarisha ufuatiliaji wa wahisiwa kwa kutuma timu ya wataalamu kwenye maeneo yenye wagonjwa wengi na utoaji wa elimu kwa jamii.

Waziri ummy amesema dalili za ugonjwa wa surua ni homa na vipele vinavyoweza kuambatana na kikohozi, macho kuwa mekundu na vidonda mdomoni, hivyo amewataka wananchi wafike vituo vya afya wanaona dalili hizo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted