Watu sita wapoteza maisha kwenye ajali mkoani Manyara

Kamanda wa Polisi wa Mkoani humo, George Katabazi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema gari hilo lilikuwa linatoka Matui kwenda Kondoa mkoani Dodoma.

0

Watu sita wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Chekanao wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Kamanda wa Polisi wa Mkoani humo, George Katabazi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema gari hilo lilikuwa linatoka Matui kwenda Kondoa mkoani Dodoma.

Kamanda Katabazi amesema ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Septemba 19 mapema asubuhi.

Amesema gari hilo la abiria lilikuwa linatokea Matui wilayani Kiteto likielekea Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

“Gari hilo mini basi lililokuwa linatokea Matui lilipata ajali eneo la Chekanao kata ya Kiperesa wakati likielekea Wilayani Kondoa mkoani Dodoma” amesema Katabazi.

Amesema miili ya marehemu na majeruhi hao ipo kwenye hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted