Dk.Mollel:Hakuna Ebola Tanzania

Serikali ya Tanzania imesema hakuna mgonjwa wa Ebola aliyeripotiwa nchini humo huku  ikiwashauri wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

0

Serikali ya Tanzania imesema hakuna mgonjwa wa Ebola aliyeripotiwa nchini humo huku  ikiwashauri wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Jana nchi ya Uganda ilitangaza mlipuko huo baada ya watu sita kufariki huku mgonjwa mmoja vipimo vya maabara kuthibitisha kuwa anaugua ugonjwa huo katika Wilaya ya Mubende iliyopo katikati ya nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa leo Septemba 21, 2022 na Naibu Waziri wa Afya nchini Tanzania, Dk Godwin Mollel imesema kuwa “Wizara inapenda kuwajulisha kwamba hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini,

Aidha imewashauri wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi na sabuni, kuepuka kugusa mwili au majimaji ya mwili wa mhisiwa au mgonjwa wa Ebola, na kuepuka safari zisizo za lazima kutembelea maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huu” imesema taarifa hiyo.

Dk Mollel amewaagiza waganga wakuu wa mikoa na halmashauri nchini kuimarisha utoaji wa elimu, ufuatiliaji wa ugonjwa, uchunguzi wa kitaalam na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba.

“Nimewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini kuimarisha utoaji wa elimu, ufuatiliaji wa ugonjwa, uchunguzi wa kitaalam na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba na kinga muhimu katika maeneo yao. Vilevile, nimewaelekeza kuimarisha uchunguzi wa wageni wanaoingia nchini kupitia mipaka yetu ikiwemo matumizi ya vipima joto (thermal scanners)”.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted