Makamba: Ni asilimia 8 tu ya Watanzania ndio wanaotumia nishati safi ya kupikia

Makamba ameyasema hayo leo Oktoba 12, 2022 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ambapo amesema zaidi ya Watanzania 33,000 hufariki kila mwaka kutokana kupumua moshi unaotokana na matumizi...

0

Waziri wa Nishati nchini Tanzania, January Makamba amesema Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 10 kusambaza gesi majumbani na viwandani ili kupambana na athari zinazotokana na matumizi ya nishati isiyo salama majumbani.

Makamba ameyasema hayo leo Oktoba 12, 2022 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ambapo amesema zaidi ya Watanzania 33,000 hufariki kila mwaka kutokana kupumua moshi unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Ameongeza kuwa uchambuzi wa matumizi ya nishati nchini unaonyesha 8% pekee ya Watanzania hutumia nishati safi ya kupikia isiyotoa moshi unaoangamiza afya zao, huku asilimia 70 ya magonjwa nchini yakiwa ni magonjwa ya mfumo wa upumuaji.

Waziri Makamba amesema ili kupambana na hayo Serikali imeandaa mjadala wa kitaifa utakaoleta suluhu ya namna ya upikaji kwa Watanzania ambao utawezesha kuweka mifumo ya kisera, mifumo ya kisheria, kikodi  na kiutawala ili kuondokana na matumizi yasiyo salama.

Kongamano hilo litakuwa na madhumuni matano ambayo ni kufahamu hali ya sasa ilivyo ya nishati ya kupikia na upikaji, kubadilishana uzoefu, ujuzi na fursa zitakazoweza kuondokana na kutatua changamoto za upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, kupitia na kujadili sera, sheria pamoja na mikakati ya kifedha na kiteknolojia itakayowezesha kuelekea kwenye nishati safi na salama, kutafuta namna bora ya kufikia malengo hayo na kutengeneza ushirikiano, maelewano na mwendo wa pamoja miongoni mwa wadau.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted