Bodi ya Mikopo Tanzania yaendelea kuandamwa, yadaiwa kutoa mikopo ya shilingi bilioni 1 kwa wanafunzi wasiostahili.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (PAC) imebaini utoaji wa mikopo inayofikia shilingi bilioni 1.76 kwa wanafunzi wasiostahili katika kipindi  cha kati ya mwaka 2016...

0

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (PAC) imebaini utoaji wa mikopo inayofikia shilingi bilioni 1.76 kwa wanafunzi wasiostahili katika kipindi  cha kati ya mwaka 2016 hadi mwaka 2018.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Japhet Hasunga ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2021.

Amesema mikopo hiyo ilitolewa kati ya mwaka 2016 hadi 2018 kwa wanafunzi ambao hawakuwa kwenye vyuo vya elimu ya juu lakini walipewa mikopo kwa maelekezo ya Serikali

Hasunga amesema uchambuzi wa taarifa ufanisi kuhusu upangaji na ugawaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kumeonekana uwepo wa maboresho makubwa katika taratibu za utoaji wa mikopo na ongezeko la idadi ya wanufaika wa mikopo husika.

Pia kumekuwa na ongezeko la wanufaika wa mikopo kutoka 116,706 (2016/2017) hadi 149,389 (2020/2021).

Alisema upangaji wa mikopo usiotosheleza kwa wanafunzi wapya ambapo Bodi haikuweza kutoa mikopo kwa asilimia 100 kwa waombaji waliostahili.

Alisema walibaini pia waombaji kupangiwa ada chini ya kiwango na zaidi ya kiwango cha ada stahiki na kwamba mwaka 2018/2019 wanafunzi 6,182 walipangiwa mikopo zaidi ya kiwango kwa kiasi cha shilingi bilioni 5.66.

Kwa mujibu wa  Hasunga ni kwamba  wanafunzi 2,852 walipangiwa mikopo chini ya kiwango kwa upungufu wa shilingi bilioni 1.14 na upangaji wa mikopo inayofikia shilingi bilioni  2.25 kwa waombaji wasiokuwa na uhitaji.

“Kutowapangia mikopo wanafunzi wanaostahili kupata mikopo na usimamizi hafifu wa bakaa na fedha za wanafunzi wanaohama vyuo na uhamasishaji duni wa vyanzo vingine vya fedha kwa ajili ya mpango wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,” amesema.

Taarifa hii inakuja wakti ambapo bado mjadala mkali uanendelea juu ya bodi ya mikopo inavyoendeshwa huku wabunge wakitaka bodi hiyo ivunjwe.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted