Tanzania yatuma wanajeshi kuzima moto mlima Kilimanjaro

Moto huo ulianza tarehe 21 mwezi oktoba karibu na eneo la Karanga linalotumiwa sana na wanaokwea mlima huo.

0
Mamia ya watu waliojitokeza kuzima moto uliokuwa unatekeza mlima Kilimanjaro nchini Tanzania mwaka wa 2020-File

Taifa la Tanzania limewatuja maafisa wa kijeshi kuwasaidia raia na watu waliojitolea kuzima moto unaosambaa kwa kasi kileleni mwa mlima Kilimanjaro ambayo imeendelea kwa siku 10 sasa.

Moto huo ulianza tarehe 21 mwezi oktoba karibu na eneo la Karanga linalotumiwa sana na wanaokwea mlima huo, takriban mita 4,000 kaskazini mwa mlima huo.

Tangu kuanza moto huo umesambaa katika maeneo mengine na kuwalemea watu takribana 600, wakiwemo wanafunzi wanaotumia matawi ya miti kuuzima.

“Maafisa hao tayari wamefika mlimani na wako tayari kuanza kuuzima,” Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) limesema katika taarifa yake bila kutoa idadi kamili.

Serikali wiki jana ilifikiri moto huo ulikuwa umedhibitiwa kabla ya upepo mkali kuenea katika maeneo mengine matatu.

“Tutashirikiana na vikosi vingine na watu wa kujitolea kuhakikisha kuwa moto unadhibitiwa haraka kabla haujaleta madhara makubwa” ilisema TPDF

Hadi kufikia sasa, hakuna majeruhi au vifo vilivyoripotiwa na utalii haujaathiriwa, hayo ni kulingana na serikali ya Tanzania.

Kilomita mbili had inane mraba wa pori umeteketezwa na moto huo, wizara ya maliasili na utalii ilisema wiki iliyopita.

Mlima huo wa Kilimanjaro ambao una theluji kilele, unasifika kote ulimwenguni. Uko kaskazini-mashariki mwa nchi ya Tanzania na ni mlima mrefu zaidi ulimwenguni ukiwa mita 5,895.

Misitu inayoizunguka ni sehemu ya hifadhi ya taifa, na hifadhi ya kitaifa ya Kilimanjaro imeorodheshwa kama eneo la urithi wa Dunia wa UNESCO, kwa sehemu kwa sababu viumbe vingi vilivyo hatarini huishi mumo.

Maafisa bado hawajagundua jinsi moto huo ulianza, lakini inakuja miaka miwili baada ya moto mwingine ambao ulianza kwa wiki moja oktoba mwaka 2020.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted