Polisi nchini Tanzania watiwa mbaroni wakidaiwa kusafirisha wahamiaji haramu.

Polisi watano wa kituo kidogo cha Uyole jijini Mbeya nchini Tanzania wamekamatwa kwa tuhuma za kula njama na kutaka kusafirisha wahamiaji haramu sita raia wa Ethiopia.

0

Polisi watano wa kituo kidogo cha Uyole jijini Mbeya nchini Tanzania wamekamatwa kwa tuhuma za kula njama na kutaka kusafirisha wahamiaji haramu sita raia wa Ethiopia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 3, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoani humo  wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 20, 2022.

Amesema kuwa Jeshi hilo lilipata taarifa za siri kutoka kwa raia wema na kutaja namba za gari lililotumika kuwasafirisha wahamiaji hao kutoka Mbeya mjini kwenda Wilaya ya Kyela mpakani wa Tanzania na Malawi, gari ambalo ni mali ya askari ambaye ni miongoni mwa wanaoshikiliwa.

Kamanda Kuzaga amewataja askari wengine na namba zao kuwa ni ASP Thomas Mbwile, G 3132 Koplo Beda, G 3146, Koplo Mohammed, G6364 Koplo Joseph wote wa Kituo cha Polisi Uyole

Amesema kuwa watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi na watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika.

“Natoa ovyo kwa watumishi wa Serikali ambao wanajihusisha na tabia ya kusafirisha wahamiaji haramu watambue kuwa Jeshi ka Polisi halijalala na watawajibishwa kwa mujibu wa Sheria”amesema.

Kwa upande wake Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Kigongo Shile amesema kuwa suala la wahamiaji haramu ni mtambuka na linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi.

“Hatutawafumbia macho watumishi wa Serikali wanaojihusisha na biashara hizo kwani Serikali imekuwa ikitumia mbinu za kuwabaini wao wanatumia mwanya kwa maslai yao binafsi.”amesema

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted