Wabunge nchini Ghana wamhoji waziri wa fedha

Serikali ya rais Nana Akufo-Addo inakabiliwa na ukosoaji unaojiri wakati ambapo serikali yake inajadiliana hadi dola bilioni 3 za mkopo kutoka kwa shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)...

0
Waziri wa fedha wa Ghana Ofori-Atta

Waziri wa fedha wa Ghana Kenneth Ofori-Atta amekabiliwa na maswali kutoka kwa wabunge kuhusu usimamizi wake wa fedha siku ya ijumaa huku serikali ikikabiliwa na shinikizo la kuongezeka kwa matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo.

Serikali ya rais Nana Akufo-Addo inakabiliwa na ukosoaji unaojiri wakati ambapo serikali yake inajadiliana hadi dola bilioni 3 za mkopo kutoka kwa shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kusaidia kufadhili fedha za umma.

Akufo-Addo mwezi uliopita alitoa wito kwa Waghana kuunga mkono juhudi zake za kudhibiti mgogoro kwani mfumuko wa bei umefikia asilimia 40 na sarafu ya taifa, na kwamba sarafu ya kitaifa cedi imesuasua sana.

Kamati ya bunge siku ya ijumaa ilikuwa ikijadili iwapo itamkashifu Ofori-Atta ambaye baadhi ya wabunge wa chama tawala tayari wamemtaka rais amtimue.

Wabunge wa upinzani walikuwa wakimhoji kuhusu madai ya matumizi mabaya ya fedha za umma na uzembe wa kutisha na kutokuwa na uwezo wa kutisha na kusababisha kuporomoka kwa uchumi wa Ghana kulingana na hoja walivyowasilisha.

Katika usemi wake wa utangulizi, Ofori-Atta alisema alitaka kuondoa shaka kuhusu umahiri wake, lakini akawaomba radhi Waghana kwa mapambano waliyokumbana nayo.

“Ninakubali uchumi wetu unakabiliwa na matatizo na watu wa Ghana wanavumilia matatizo,” alisema.

“Kama mtu ambaye rais Akufo-Addo amemweka kusimamia uchumi huu, ninahisi uchungu binafsi, kitaaluma na katika nafsi yangu,”

Hashitagi #KenMustGo ilikuwa ikivuma kwenye mtandao wa twita.

Kamati ya bunge itachunguza madai dhidi ya waziri huyo kabla ya kuamua kuwasilisha hoja ya kushutumu bunge, ambayo imegawanyika katikati baina ya chama tawala cha NPP na chama cha upinzani cha NDC.

Hata hivyo rais mwenyewe ndio atatoa uamuzi wa mwisho wa kumfukuza waziri au la.

Mapema wiki hii Akufo-Addo alimfuta kazi waziri mdogo wa fedha wa serikali, Charles A du Boahen, kutokana na tuhuma za ufisadi baada ya kuonekana kwenye filamu ya ufichuzi.

Akufo-Addo pia alipeleka kesi hiyo kwa waendesha mashataka kwa uchunguzi zaidi.

Kiongozi huyo wa Ghana mwaka huu alibadili msimamo wake na kusema atatafuta mkopo wa IMF baada ya serikali yake kusema awali kwamba ushuru mpya wa miamala ya kielekroniki utasaidia nchi hiyo kuepuka mkopo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted