Hakimu adaiwa kujiua kwa kunywa sumu akiwa gesti

Akizungumzia tukio hilo jana Novemba 29, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya amesema tukio hilo limetokea Novemba 27 mwaka huu akiwa amelala katika nyumba ya wageni.

0

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Michael Royan (31) anadaiwa kujiua kwa kunywa sumu katika nyumba ya kulala wageni ya ‘gesti’ iliyopo Manispaa ya Sumbawanga mkoani humo.

Akizungumzia tukio hilo jana Novemba 29, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya amesema tukio hilo limetokea Novemba 27 mwaka huu akiwa amelala katika nyumba ya wageni.

Amesema kuwa asubuhi ya siku hiyo ofisa upelelezi wa mkoa wa Rukwa alipigiwa simu na mmiliki wa nyumba hiyo na kueleza kuwa kuna mteja ambaye amelala na hajaamka na inaonekana kuwa amepoteza fahamu.

Kamanda Mallya amesema baada ya polisi kufika eneo hilo waliingia ndani ya chumba hicho na kumchukua mtu huyo kisha kumpeleka hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Sumbawanga ambapo alipokelewa na baada ya uchunguzi wa awali wa kitabibu ilibainika kuwa mtu huyo amefariki dunia.

Amesema kuwa Polisi walipoanza uchunguzi wa tukio hilo walibaini kuwa marehemu alikua ni mtumishi wa Serikali katika idara ya mahakama mkoani hapa katika mahakama ya mwanzo na kituo chake kilikuwa ni Mahakama ya mwanzo Kasanga.

Kamanda huyo amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa huenda marehemu alikunywa sumu, lakini baadhi ya viungo vyake vya mwili vimechukuliwa na kupeleka sampuli kwa mkemia mkuu ili kupata majibu sahihi ya nini kilicho sababisha kifo cha Hakimu huyo.

Amesema marehemu hakuacha ujumbe wowote hivyo imekua ni vigumi kufahamu sababu za tukio hilo lakini amedai kuwa jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na litatoa taarifa baada ya uchunguzi huo kukamilika.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted