Sherehe za uhuru nchini Tanzania kufanyika kivingine

Akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 5,2022 ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka...

0

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza shilingi milioni 960 zilizotengwa na Wizara na Taasisi kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru mwaka huu, zipelekwe Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika shule nane za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 5,2022 ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 zitafanyika kwa njia ya midahalo na makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika wilaya zote hapa nchini.

“Midahalo na makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa,”– amesema Simbachawene.

Ameongeza kuwa “Midahalo na Makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa.”

Simbachawene amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 yataadhimishwa kwa Kauli mbiu inayosema:- MIAKA 61 YA UHURU: AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU.

Waziri huyo ameongeza kuwa kauli mbiu hiyo inaonyesha nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha uchumi unaojikita katika maendeleo ya watu kwa kufanya mabadiliko katika sekta zote za kiuchumi na kijamii ili kufikisha neema na Maendeleo

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted