Rais Ruto Atumia “Minofu Ya Maendeleo” Kuinasa Nyanza .

Rais wa Kenya WIlliam Ruto na naibu rais Rigathi Gachagua Jumanne asubuhi Wameandaa kikao na viongozi kutoka eneo la Nyanza katika ikulu ya Nairobi kufuatia ziara yake ya...

0

Viongozi wa eneo la nyanza wakikutana na rais William Ruto Ikulu.(Hisani ya picha-Ikulu )


Rais wa Kenya WIlliam Ruto na naibu rais Rigathi Gachagua Jumanne asubuhi Wameandaa kikao na viongozi kutoka eneo la Nyanza katika ikulu ya Nairobi kufuatia ziara yake ya hivi majuzi katika eneo hilo.


Viongozi waliohudhuria kika cha ikulu ni pamoja na seneta wa kaunti ya kisumu Tom Ojienda,wabunge Shakeel Shabir (Kisumu Mashariki), Mark Nyamita (Uriri), Elisha Odhiambo (Gem), Gideon Ochanda (Bondo), John Owino (Awendo) Felix Odiwuor ambaye wengi wanamjua kama Jalang’o(Lang’ata)Paul Abuor (Rongo) , John Owino (Awendo).


Rais Willia Ruto amedokeza kuwa aliandaa kikao hiki ili kuzungumza na viongozi hao jinsi watashirikiana kufanikisha maendeleo eneo hilo kwa faida ya wakaazi.


“Viongozi wanafaa kuungana na kushirikiana katika utendakazi wao ili kupambana na changamoto zinazolikumba taifa hili.Wanafaa kuwa mfano bora kwa kufanikisha majukumu waliotwikwa na wananchi kwa kuwachagua.Hii ni njia bora ya kuendeleza umoja wa taifa la Kenya”alisema Rais William Ruto.


Rais William Ruto alisema kuwa kikao chake kilijikita katika hatua ya maendeleo ambayo imefanikishwa eneo hilo siku chache baada ziara yake ambapo alizundua baadhi ya miradi ikiwemo ule nyumba 5,000 za bei nafuu kaunti ya Homa bay.


Katika ziara yake hivi majuzi eneo la nyanza Rais Ruto alitoa aahadi ya serikali yake ya kenya kwanza kujenga soko la samaki ambalo litagharimu Sh600 milioni kaunti ya Homabay ,soko ambalo litawafaa wakaazi kwa kuwa na kiwanda cha samaki ikizingatiwa kuwa uvuvi ni kitega uchumi eneo la Nyanza.


Minofu ya maendeleo ambayo rais Ruto amekuwa akiwapa na kuwahidi wananchi wa Nyanza ni baadhi ya mbinu ambayo wadadisi wa siasa wanahoji kuwa anatumia kuvua ufuasi wa ene hilo ambalo limekuwa ngome ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted