Uganda yawafunga wakenya miaka 20 jela kwa kutumia silaha kinyume cha sheria

Wafugaji hao 32 walikamatwa katika operesheni ya kijasusi siku ya Jumamosi, kufuatia majibizano ya risasi katika wilaya ya Moroto kaskazini mashariki mwa Uganda

0

Mahakama ya kijeshi nchini Uganda imewahukumu makumi ya wafugaji wa Kenya kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukiri kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria, afisa mmoja alisema Alhamisi.

Wafugaji hao 32 wa kuhamahama kutoka kaskazini mwa Kenya walikamatwa katika operesheni ya kijasusi siku ya Jumamosi, kufuatia majibizano ya risasi katika wilaya ya Moroto kaskazini mashariki mwa Uganda, Brigedia Jenerali Joseph Balikuddembe alisema.

Walifikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi siku ya Jumanne, afisa huyo wa mjini Moroto alisema.

“Washukiwa hao 32 walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kukiri kosa lao la kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria,” alisema.

Eneo hilo la kaskazini-mashariki limevumilia miongo kadhaa ya uvamizi wa ng’ombe wenye silaha kati ya koo za wahamaji ambao wanazunguka kwenye mpaka usio na sheria kati ya Uganda, Sudan Kusini na Kenya.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted