#KENYA: Mwanamke anayedaiwa kumuua na kula sehemu za mwili wa mtoto wake amezuiliwa kwa siku 10

"Ninajichukia mwenyewe. Sijipendi ndio maana niliuawa mtoto wangu. Nimepitia magumu na huyu mtoto," mwanamke huyo alisema

0

Mwanamke mmoja alilazwa Jumatatu katika hospitali ya Kitengela baada ya kumvamia na kumuua bintiye wa miaka miwili.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 alianguka na kupelekwa hospitalini baada ya shambulio hilo la kutisha ambalo lilinaswa kwenye video na majirani.

Katika kile kinachodhaniwa kuwa ni ukatili unaohusishwa na ugonjwa wa akili, mwanamke huyo alisema alimshambulia mtoto wake kwa sababu anajichukia na ameteseka sana na mtoto wake.

“Ninajichukia mwenyewe. Sijipendi ndio maana niliuawa mtoto wangu. Nimepitia magumu na huyu mtoto,” mwanamke huyo alisema.

Wakati wa shambulio la Jumapili usiku, majirani walitazama kwa hofu huku mwanamke huyo, mwanafunzi wa Biashara katika chuo kikuu cha eneo hilo, akimdunga kisu mtoto huyo na kumkatakata.

Majirani hao walikimbilia kwenye nyumba hiyo baada ya kusikia mayowe wakishuku wahalifu walivamia nyumba hiyo na kumpata mama huyo mdogo akiwa uchi huku akimshambulia kwa nguvu bintiye.

Wazazi wa mama huyo ambao wanaishi nyumba moja hawakuwapo nyumbani wakati wa tukio hilo.

Majirani walipofanikiwa kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba, mtoto huyo alikuwa tayari amekufa na mama yake alikuwa ameanguka. Nyumba hiyo ilikuwa na samani nyingi na vifaa vya elektroniki vilivyoharibiwa.

Polisi huko Kitengela wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Mkurugenzi wa DCI wa Kitengela Benson Mutia alisema mama huyo atafikishwa mahakamani baada ya polisi kumhoji.

“Ni tukio la kushangaza. Tutakuwa tukimhoji ili kufahamu kiini cha mauaji hayo. Pia tunataka kujua ikiwa mauaji hayo yalikusudiwa,” alisema.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted