Majaliwa awataka Watanzania kuiombea Yanga irudi na ushindi

Akizungumza leo bungeni Jijini Dodoma Majaliwa amesema ni wakati wa Watanzania wote kuungana ili kuandika historia kwa pamoja na hana shaka na uwezo wa Yanga, na anaamini timu...

0

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuungana kwa pamoja kuiombea timu ya Yanga kwenye mchezo wa ingwe ya pili ya fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya USM Alger utakaopigwa Juni 3 nchini Algeria.

 Akizungumza leo bungeni Jijini Dodoma Majaliwa amesema ni wakati wa Watanzania wote kuungana ili kuandika historia kwa pamoja na hana shaka na uwezo wa Yanga, na anaamini timu hiyo itaipeperusha vyema bendera ya Tanzania 

“Timu yetu ina uwezo mkubwa hivyo tuiombee, niungane na watanzania wenzangu kumshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutoa usafiri kwa Yanga, Mwenyezi Mungu awatangulie ili wakaandike historia” 

Yanga wameondoka hapa nchini leo Juni 1 kwenda nchini Algeria kwa ajili ya mchezo huo ambapo wanahitaji ushindi wenye faida kwao ili kuwa mabingwa wa kombe la shirikisho Afrika.

Wakiwa nyumbani Yanga ilifungwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Mkapa Mei 28, matokeo hayo yanaipa nafasi nguumu Yanga katika mchezo wao Juni 3 nchini Algeria.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted