Serikali ya Zanzibar yatangaza rasmi umiliki wa Shamba la Razaba huko Bagamoyo, yatoa onyo kwa wenye kutaka kujimilikisha

Taarifa iliyotolewa na  serikali ya Zanzibar, kupitia kwa msemaji wake, Charles Hilary, imeeleza kuwa shamba hilo ni mali ya serikali na haitambui mtu yoyote aliyemilikishwa; au kujimilikisha eneo...

0

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba la Razaba lilipo eneo la Bagamoyo, mkoani Pwani, ni mali halali ya serikali hiyo. 

Taarifa iliyotolewa na  serikali ya Zanzibar, kupitia kwa msemaji wake, Charles Hilary, imeeleza kuwa shamba hilo ni mali ya serikali na haitambui mtu yoyote aliyemilikishwa; au kujimilikisha eneo hilo.

“Eneo la shamba la Makurunge, Razaba, lililopo wilaya ya Bagamoyo, kata ya Makurunge, lenye ukubwa wa takribani hekta elfu sita, ni mali ya Serikali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, tangu mwaka 1977.” Charles Hilary, Msemaji wa Serikali ya Zanzibar.

Serikali hiyo imepiga marufuku  kwa mtu, taasisi au kikundi chochote kufanywa shughuli yoyote katika eneo hilo kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa na pia hakutakuwa na fidia yoyote kwa mtu aliyepatiwa eneo katika shamba hilo

“Hivyo ni marufuku kwa mtu, taasisi au kikundi chochote, kufanya shughuli yoyote katika eneo hilo. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kikundi cha watu, kitakachokwenda kinyume na tangazo hilo. serikali haitakuwa na wajibu wa kulipa fidia kwa mtu yoyote aliyepatiwa eneo katika shamba hilo.”

Aidha, taarifa hiyo inasema, Mgogoro kati wananchi wa kijiji cha Winde na Ranchi ya Razaba, umedumu kwa zaidi ya miaka 40 sasa, kufuatia baadhi yao kudai kuwa eneo lao lilichukuliwa na Serikali ya Zanzibar, bila ridhaa yao na bila kulipwa fidia.

Lakini Razaba wanadai kuwa kabla ya kulichukua eneo hilo, ambalo lilikuwa likitumika kwa ajili ya kufungia ng’ombe kabla ya kusafirishwa Zanzibar, walilipa mamilioni ya fedha kama fidia kwa wananchi hao.

Ramani ya eneo la Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA)

Ranchi ya RAZABA ilianzishwa Oktoba mwaka 1977 kwa makubaliano ya pande mbili kati ya serikali ya Zanzibar na serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambapo jumla ya  hekari 77,663 zilikabidhiwa kwa serikali ya Visiwani, kupitia iliyokuwa wizara ya kilimo na maliasili.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted